Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g04 7/8 uku. 3
  • Kubalehe Ni Kipindi Kizuri na Kigumu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kubalehe Ni Kipindi Kizuri na Kigumu
  • Amkeni!—2004
  • Habari Zinazolingana
  • Kubalehe—Kujitayarisha Kuwa Mtu Mzima
    Amkeni!—2011
  • Kuwatayarisha Vijana kwa Ajili ya Maisha ya Utu Uzima
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Utafanya Nini Kijana Wako Akitilia Shaka Imani Yako?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2004
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2004
g04 7/8 uku. 3

Kubalehe Ni Kipindi Kizuri na Kigumu

KUBALEHE kunaweza kuwa kipindi kizuri sana maishani. Vijana wengi hufurahia kipindi hicho. Na watu wazima wengi wanakumbuka jinsi walivyofurahia miaka yao ya ujana.

Wakati huohuo, ni lazima tutambue kwamba tunaishi katika “nyakati za hatari zilizo ngumu kushughulika nazo.” (2 Timotheo 3:1) Hilo limewaongezea vijana mkazo mwingi kuliko ule ambao vijana walikabili zamani. Huenda ndiyo sababu Sabrina Solin Weill, mhariri mkuu wa gazeti moja la vijana, alisema kwamba kubalehe ni kama “kutembea juu ya kamba iliyoning’inizwa hewani bila kitu cha kukukinga unapoanguka chini.” Kwa kweli, kipindi hicho kigumu maishani kinaweza kumfanya mtu akose uhakika, awe na wasiwasi mwingi, na kuvurugika sana. Weill anaandika: “Vijana wanaobalehe hukabili magumu ya utoto na utu uzima.”

Ikiwa wewe ni kijana anayebalehe, utakabilianaje na magumu hayo? Ikiwa wewe ni mzazi wa kijana anayebalehe, ni nini kinachoweza kukusaidia kukumbuka jinsi miaka hiyo migumu ilivyokuwa ili uelewe vizuri yale ambayo mwana au binti yako anakabili? Katika mfululizo huu, tunawaomba vijana na watu wazima kuchunguza kwa makini kipindi cha kubalehe. Kufanya hivyo kutawasaidia vijana kuvumilia na hata kufanikiwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki