Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g04 7/8 uku. 32
  • Mama Mwenye Ufahamu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mama Mwenye Ufahamu
  • Amkeni!—2004
Amkeni!—2004
g04 7/8 uku. 32

Mama Mwenye Ufahamu

Mama anayefahamu na anayejali mahitaji ya watoto wake hujitahidi kwa bidii kuwaandalia chakula cha kimwili kinachoboresha afya. Yeye hujitahidi vivyo hivyo kushughulikia mahitaji yao ya kiroho.

Hivi majuzi, mwanamke mmoja huko Brazili, aliiandikia ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova katika nchi hiyo ili kuonyesha uthamini wake kwa broshua Mungu Anataka Tufanye Nini? “Broshua hiyo ilinivutia sana,” akaandika. “Nilipotazama lile somo linalozungumzia mazoea ambayo Mungu huchukia, nilitambua mara moja kwamba ninapaswa kuzungumzia habari hiyo ya maana pamoja na watoto wangu—binti wawili, mmoja mwenye umri wa miaka 10 na mwingine miaka 11, na mvulana wa miaka 5.” Aliongezea: “Ni muhimu sana kuwa na vitabu kama hivi vya kufundisha familia yangu kumhusu Mungu!”

Pia aliomba vitabu zaidi vya Biblia. Ikiwa wewe pia unatamani chakula cha kiroho, kwa ajili yako na familia yako, unaweza kupata nakala ya Mungu Anataka Tufanye Nini? Jaza sehemu iliyo hapa chini na uitume ukitumia anwani iliyoonyeshwa au anwani ifaayo kati ya zile zilizoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5 wa gazeti hili.

□ Ningependa kupokea broshua Mungu Anataka Tufanye Nini? bila malipo. Andika lugha unayotaka.

□ Ningependa kujifunza Biblia nyumbani kwangu bila malipo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki