Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g05 3/8 uku. 32
  • Unakaribishwa kwenye Mkutano Muhimu Zaidi wa Mwaka!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Unakaribishwa kwenye Mkutano Muhimu Zaidi wa Mwaka!
  • Amkeni!—2005
Amkeni!—2005
g05 3/8 uku. 32

Unakaribishwa kwenye Mkutano Muhimu Zaidi wa Mwaka!

Mnamo Alhamisi, Machi 24, 2005, kutakuwa na tukio ambalo hupaswi kukosa. Hiyo ndiyo siku ambayo zaidi ya Mashahidi wa Yehova milioni sita ulimwenguni pote hukusanyika pamoja na mamilioni ya marafiki wao ili wakumbuke mlo wa jioni wa mwisho ambao Yesu alikuwa nao pamoja na wanafunzi wake. Kulingana na maagizo ya Yesu, mkate usiotiwa chachu pamoja na divai nyekundu zitapitishwa katika kila mkutano, na maana ya sherehe hiyo itaelezwa. —Marko 14:22-24.

Watu wengi wanafahamu tukio hilo kuwa Mlo wa Jioni wa Bwana. Mashahidi wa Yehova huliita Ukumbusho wa kifo cha Kristo. Tukio hilo ni muhimu ili kukumbuka dhabihu ambayo Yesu Kristo alitoa kwa ajili ya wanadamu wenye dhambi alipokufa. (Yohana 3:16; 1 Yohana 2:2) Baada ya mlo huo wa mwisho, Yesu alikamatwa na baadaye akafa juu ya mti kana kwamba alikuwa mtenda-dhambi wa kawaida. —Yohana 19:17, 18.

Unakaribishwa kwa uchangamfu uhudhurie mkutano huo wa pekee wa kila mwaka ambao ndio mkutano muhimu zaidi kwa Mashahidi wa Yehova. Tafadhali nenda kwenye Jumba la Ufalme lililo karibu nawe ili ujue saa na mahali ambapo mkutano huo utafanyiwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki