Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g05 12/8 uku. 32
  • Anakumbuka Mambo Muhimu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Anakumbuka Mambo Muhimu
  • Amkeni!—2005
Amkeni!—2005
g05 12/8 uku. 32

Anakumbuka Mambo Muhimu

Alipopata kitabu Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu, mwanamke mmoja aliamua kumpelekea dada yake mkubwa nakala moja. Dada yake aliye na umri wa miaka 80 na kitu anaugua ugonjwa wa Alzheimer. Hata hivyo, kwa miaka 70 amekuwa mwanafunzi na mwalimu wa Biblia mwenye bidii. Lakini yeye hukumbuka matukio machache ya karibuni naye huzungumza mara chache.

“Siku ya kwanza,” dada mdogo alieleza, “nilimweleza kwamba kitabu hicho kimeandikwa katika njia ambayo kinaweza kuwasaidia wazazi kukazia kanuni na mafundisho ya Biblia katika mioyo ya watoto wao na kwamba ningependa kumsomea. Hakunijibu. Hata hivyo, nilipoanza kusoma, alisisimka na kujibu kila swali nilipokuwa nikisoma. Nyakati nyingine nilipokuwa nikisoma andiko alilimalizia kutoka kwa kumbukumbu, lakini akinukuu Biblia ya King James Version, ambayo alisoma alipokuwa kijana. Mara kwa mara, alinishika mkono nilipokuwa nikisimulia simulizi la Biblia na kusema, ‘Ala, ninakumbuka jambo hilo!’

“Baada ya kumsomea zaidi ya nusu ya kitabu hicho, wakati wangu wa kuondoka ulifika naye dada yangu akasema kwamba angependa kusikia zaidi. Mume wake, ambaye humtunza vizuri sana, aliendelea kumsomea sehemu iliyobaki ya kitabu hicho. Jambo hilo lilinisaidia kutambua umuhimu wa kuwasomea wazee na walio dhaifu vichapo kama hivyo.

Vijana na wazee hufurahia kusoma kitabu hicho chenye kurasa 256 chenye picha zenye kuvutia, na ukubwa kama wa gazeti hili. Ingawa masomo yanayotegemea mafundisho ya Yesu Kristo yameelezwa kwa kutumia lugha rahisi, habari yenyewe inafaa watu wa umri wote. Unaweza kuomba kitabu hicho kwa kujaza sehemu iliyo hapa chini na kuituma ukitumia anwani iliyoonyeshwa au anwani ifaayo kati ya zile zilizoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5 wa gazeti hili.

□ Ningependa kupokea kitabu Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu bila malipo.

□ Ningependa kujifunza Biblia nyumbani kwangu bila malipo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki