Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 10/08 uku. 3
  • Je, Mtoto Wako Anatumia Intaneti?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Mtoto Wako Anatumia Intaneti?
  • Amkeni!—2008
  • Habari Zinazolingana
  • Watoto na Intaneti—Mambo Ambayo Wazazi Wanaweza Kufanya
    Amkeni!—2008
  • Kuwasaidia Vijana Wakabiliane na Hali Ngumu
    Amkeni!—2007
  • Kuna Ubaya Kufanya Urafiki Kupitia Intaneti?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
  • Watoto na Intaneti—Mambo Ambayo Wazazi Wanapaswa Kujua
    Amkeni!—2008
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2008
g 10/08 uku. 3

Je, Mtoto Wako Anatumia Intaneti?

WAKATI wowote ule, mamilioni ya vijana wanatumia Intaneti, iwe nyumbani, shuleni, kwenye nyumba ya rafiki, au, ikiwa wana Intaneti kwenye simu zao za mkononi au vifaa vingine kama hivyo, wanaweza kuitumia mahali popote pale. Ikiwa wewe ni mzazi, basi unakabili jambo zito: Huenda watoto wako wanaelewa sana ulimwengu wa Intaneti kuliko wewe, na hata wanaweza kukuficha mambo wanayofanya kwenye Intaneti.

Je, jambo hilo linapaswa kukuhangaisha? Bila shaka. Je, kuna suluhisho? Ndiyo. Ni kweli kwamba huenda ikaonekana kwamba mtoto wako ni mwenyeji wa Intaneti na wewe ni mtalii tu. Hata hivyo, unaweza kujua mambo yanayohusika na si lazima uwe mtaalamu wa vifaa vya elektroniki ili kumlinda mtoto wako.

Makala hizi zitakufundisha mambo fulani muhimu. Lakini kwanza hebu tuzungumzie baadhi ya hatari ambazo mtoto wako huenda akakabili kwenye Intaneti.

[Picha katika ukurasa wa 3]

Nchini Kanada, karibu nusu ya vijana wote walio na simu za mkononi wanaweza kutumia Intaneti

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki