Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 3/09 uku. 9
  • Mdomo wa Ngisi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mdomo wa Ngisi
  • Amkeni!—2009
  • Habari Zinazolingana
  • Kiungo cha Ngisi wa Hawaii Kinachotoa Mwangaza
    Amkeni!—2015
  • Mdomo wa Toucan
    Amkeni!—2009
  • Wanyama Wakubwa wa Baharini
    Amkeni!—2009
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2009
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2009
g 3/09 uku. 9

Je, Ni Kazi ya Ubuni?

Mdomo wa Ngisi

◼ Wanasayansi wanastaajabishwa na mdomo wa ngisi. Wao hujiuliza: ‘Kitu kigumu sana hivyo kinaweza kuunganishwa kwa mwili usio na mifupa jinsi gani? Je, kuunganisha kitu kigumu na kitu chepesi hakuwezi kumchubua na kumuumiza ngisi?’

Fikiria hili: Ncha ya mdomo wa ngisi ni ngumu lakini sehemu ya chini ni laini. Mdomo huo umetengenezwa kwa mchanganyiko wa protini, maji, na kitu kigumu kinachoitwa chitin. Ugumu wa mchanganyiko huo hubadilika polepole kutoka kuwa laini hadi kuwa mgumu na hivyo ngisi anaweza kutumia mdomo wake bila kujichubua.

Profesa Frank Zok wa Chuo Kikuu cha California anasema kwamba kuchunguza mdomo wa ngisi kunaweza “kubadili sana maoni ya wahandisi kuhusu jinsi ya kuunganisha vitu mbalimbali.” Ujuzi huo unaweza kutumiwa kutengeneza viungo bandia. Ali Miserez, mchunguzi katika chuo hicho, anafikiria jinsi ya “kubuni kiungo bandia kinachoiga mchanganyiko wa mdomo huo, ili upande mmoja wa kiungo hicho uwe laini kama gegedu na upande mwingine” uwe umetengenezwa “kwa kitu kigumu.”

Una maoni gani? Je, mdomo wa ngisi wenye ncha ngumu na sehemu laini ya chini ulijitokeza wenyewe? Au ulibuniwa?

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 9]

© Bob Cranston/SeaPics.com

© Richard Herrmann/SeaPics.com

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki