Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 1/12 uku. 3
  • Ukosefu wa Unyoofu Umeenea Sana!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ukosefu wa Unyoofu Umeenea Sana!
  • Amkeni!—2012
  • Habari Zinazolingana
  • Unyoofu Huleta Mafanikio ya Kweli
    Amkeni!—2012
  • Mambo Tunayojifunza Kutokana na Maisha ya Samweli
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2022
  • Athari za Kukosa Unyoofu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2016
  • Kushinikizwa Usiwe Mnyoofu
    Amkeni!—2012
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2012
g 1/12 uku. 3

Ukosefu wa Unyoofu Umeenea Sana!

Dannya anafanya kazi katika kampuni moja kubwa nchini Hong Kong. Alipokuwa akitembelea kiwanda fulani, alieleza wasiwasi wake kwamba kiwanda hicho hakingeweza kutimiza viwango vinavyohitajiwa ili kutokeza bidhaa za kampuni yao. Baadaye walipokuwa wakila, meneja wa kiwanda hicho alimpa Danny bahasha fulani. Ndani kulikuwa na rushwa ya maelfu ya dola​—kiasi cha dola hizo kilikuwa sawa na mshahara wake wa mwaka mzima.

● Kisa cha Danny si cha kipekee. Ulimwenguni pote, ukosefu wa unyoofu umeenea sana. Kwa mfano, hati za mahakamani zinaonyesha kwamba kati ya mwaka wa 2001 na 2007, kiwanda kimoja kikubwa nchini Ujerumani kilitoa rushwa ya jumla ya dola bilioni 1.4 ili kipate kandarasi mbalimbali.

Ingawa kashfa za karibuni zinazohusisha makampuni makubwa zimefanya kuwe na mabadiliko fulani, hali kwa ujumla inaendelea kuzorota. Uchunguzi uliofanywa mwaka wa 2010 na shirika la Transparency International ulionyesha kwamba ulimwenguni pote, “viwango vya ufisadi vimeongezeka katika miaka mitatu iliyopita.”

Kwa nini kuna ukosefu mwingi wa unyoofu? Je, kuna faida zozote za kuwa mnyoofu? Ikiwa kuna faida, mtu anawezaje kuwa mnyoofu? Je, Biblia inaweza kutusaidia?

[Maelezo ya Chini]

a Baadhi ya majina katika mfululizo huu yamebadilishwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki