Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 2/12 uku. 32
  • “Kitabu Hiki Kimeandikwa kwa Ustadi Sana”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Kitabu Hiki Kimeandikwa kwa Ustadi Sana”
  • Amkeni!—2012
Amkeni!—2012
g 2/12 uku. 32

“Kitabu Hiki Kimeandikwa kwa Ustadi Sana”

● Je, ungependa kusoma kuhusu maisha ya Yesu Kristo hapa duniani, kutia ndani mafundisho yake yanayobadili maisha na mifano isiyosahaulika? Ikiwa ndivyo, unaweza kusoma kitabu Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi.

Baada ya kusoma kitabu hicho, mwanamume mmoja mwenye uthamini alisema hivi: “Ingawa kimeandikwa kwa njia rahisi, kinaeleza kwa njia yenye kuvutia kila jambo alilofanya Bwana wetu alipokuwa hapa duniani. Kwa kweli kitabu hiki kimeandikwa kwa ustadi sana.”

Kwa kadiri inavyojulikana, matukio yanayosimuliwa katika kitabu hicho yanafuata utaratibu wa jinsi yalivyotokea. Kinategemea hasa vitabu vinne vya Injili vilivyoandikwa na watu walioishi wakati uleule Yesu alipokuwa duniani wakiongozwa na roho ya Mungu, yaani, Injili ya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana. Mathayo na Yohana walikuwa mitume na walisafiri pamoja na Yesu. Marko alikuwa rafiki wa karibu wa Petro, mmoja wa mitume wa Yesu. Daktari Luka naye aliandamana na mtume Mkristo Paulo katika safari zake.

Unaweza kuomba kitabu hicho kwa kujaza sehemu iliyoonyeshwa hapa chini na uitume kwenye anwani ifaayo kati ya zile zilizoorodheshwa katika ukurasa wa 5 wa gazeti hili.

□ Bila masharti, ningependa kupokea kitabu kilichoonyeshwa hapa.

□ Ningependa kujifunza Biblia nyumbani kwangu bila malipo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki