Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 3/14 kur. 10-11
  • Kutembelea El Salvador

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutembelea El Salvador
  • Amkeni!—2014
Amkeni!—2014
g 3/14 kur. 10-11
Nchi ya El Salvador

NCHI NA WATU | EL SALVADOR

Kutembelea El Salvador

Ramani ya El Salvador

MIAKA 500 hivi iliyopita, Wahispania walipofika katika nchi ambayo sasa inaitwa El Salvador, kabila kubwa la huko liliita eneo hilo Cuscatlán—jina linalomaanisha “Nchi ya Vito.” Leo, watu wengi nchini El Salvador ni wazao wa makabila ya wenyeji na Wazungu waliohamia huko.

Wenyeji wa El Salvador wanajulikana kuwa watu wenye bidii na urafiki. Ni wenye adabu na heshima. Watu husalimiana kwa adabu kabla ya kuanza mazungumzo au wanapoingia dukani kwa kusema, “Buenos días” (habari ya asubuhi) au “Buenas tardes” (habari ya alasiri). Kwa wenyeji wa El Salvador wanaoishi vijijini na katika miji midogo, wanaona ni utovu wa adabu kumpita mtu bila kumsalimu.

A Mwanamke akikusanya buni za kahawa

Kilimo cha kahawa kimebadili sana maisha ya watu wa El Salvador

Chakula wanachopenda sana ni pupusa,​—yaani, chapati ndogo zilizotengenezwa kwa unga wa mahindi (au mchele) na kisha kujazwa jibini, maharagwe, nyama ya nguruwe, au mchanganyiko mwingine. Mara nyingi pupusa huliwa kwa mchuzi wa nyanya na curtido, yaani, mchanganyiko wa kabeji, karoti, vitunguu, na siki yenye vikolezo. Ingawa watu fulani hula chakula hicho kwa kisu na uma, wenyeji hula kwa mikono.

Pupusa

Pupusa ni moja kati ya vyakula vinavyopendwa sana nchini El Salvador

Maporomoko ya Maji ya Los Tercios

Maporomoko ya Maji ya Los Tercios huko Suchitoto

JE, WAJUA? El Salvador inaitwa nchi ya volkano. Kuna zaidi ya milima 20 ya volkano, na baadhi ya milima hiyo bado hulipuka. Maporomoko ya maji ya Los Tercios hutiririka juu ya safu ndefu za miamba iliyochongoka ambayo ilitokezwa na mlipuko wa volkano.

Kuna Mashahidi wa Yehova zaidi ya 38,000 nchini El Salvador, nao hukutana katika makutaniko 700 hivi. Wao huwafundisha watu 43,000 hivi Biblia katika lugha ya Kihispania, Kiingereza, na Lugha ya Ishara ya El Salvador.

TAARIFA FUPI

  • Idadi ya watu: 6,267,000

  • Mji mkuu: San Salvador

  • Lugha rasmi: Kihispania

  • Hali ya Hewa: Joto kali kwenye eneo la pwani na maeneo tambarare; baridi ya kiasi kwenye maeneo yaliyoinuka

  • Nchi: Ina milima mingi na eneo la katikati ya nchi ni tambarare

CHEMSHA BONGO

Jibu kweli au si kweli.

  1. El Salvador ni nchi ndogo zaidi huko Amerika ya Kati.

  2. El Salvador ni nchi yenye msongamano mkubwa zaidi wa watu katika Amerika ya Kati.

  3. Vyakula vingi vya El Salvador hutiwa vikolezo vingi.

  4. Kilimo cha kahawa kimebadili sana maisha ya watu wa El Salvador.

Majibu: A, B, na D ni kweli; C si kweli. Wageni wengi husema kwamba vyakula vya El Salvador havina vikolezo vingi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki