Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 7/14 kur. 10-11
  • Kutembelea Ireland

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutembelea Ireland
  • Amkeni!—2014
Amkeni!—2014
g 7/14 kur. 10-11
Pwani ya Ireland

NCHI NA WATU | IRELAND

Kutembelea Ireland

Ramani ya Jamhuri ya Ireland na Ireland Kaskazini

KISIWA hicho kinachoitwa pia “Emerald Isle” (Kisiwa cha Kijani) kina nchi mbili: nchi kubwa ni Jamhuri ya Ireland, na nchi ndogo ni Ireland Kaskazini, ambayo ni sehemu ya Uingereza.

Giant’s Causeway

Giant’s Causeway

Kisiwa cha Ireland kinaitwa Kisiwa cha Kijani kwa sababu kina mvua nyingi inayofanya sehemu kubwa ya nchi hiyo kuwa kijani. Mito na maziwa maridadi kutia ndani miinuko ya pwani pamoja na vilima huchangia uzuri wa nchi hiyo.

Nyumba iliyoezekwa kwa nyasi

Nyumba iliyoezekwa kwa nyasi

Wakaaji wa Ireland wamekabili shida nyingi. Kwa mfano, inakadiriwa kwamba kati ya mwaka 1845 hadi 1851, karibu watu milioni moja walikufa kwa njaa na magonjwa mimea ya viazi ilipoharibiwa na ugonjwa. Ili kukimbia umaskini mkubwa watu wengi walihamia nchi nyingine kama vile Australia, Kanada, Marekani, na Uingereza. Leo, karibu Wamarekani milioni 35 wana asili ya Ireland.

Wenyeji wa Ireland wanajulikana kuwa wachangamfu na wakarimu. Wanapenda sana mbio za farasi, michezo kama vile kriketi, raga, mpira wa miguu, na mchezo wa Gaelic (unaofanana na mpira wa miguu). Wanawake wanapenda mchezo uitwao camogie, unaofanana na mpira wa magongo.

Bendi ya wenyeji wa Ireland

Bendi ya wenyeji wa Ireland

Watu wa Ireland hupenda pia mazungumzo na muziki. Dansi ya Ireland (step dance) ni maarufu duniani kote. Wachezaji hukaza sehemu ya juu ya mwili na kuchezesha miguu yao kwa ustadi mkubwa.

Mashahidi wa Yehova wamekuwa nchini Ireland kwa zaidi ya miaka mia moja. Sasa, zaidi ya Mashahidi 6,000 huko Ireland wanawafundisha watu Biblia.

1. kinubi cha Kiselti; 2. zumari iitwayo bagpipe; 3. fidla; 4. kodiani; 5. filimbi; 6. ngoma iitwayo bodhran

Muziki wa asili wa Ireland huchezwa kwa ala zilizo hapa chini, kuanzia kushoto kwenda kulia: kinubi cha Kiselti, zumari iitwayo bagpipe, fidla, kodiani, filimbi, na ngoma iitwayo bodhran

JE, WAJUA?

Eneo la Giant’s Causeway lililo kwenye pwani ya kaskazini ya Ireland Kaskazini, lina maelfu ya nguzo za mawe zilizotokana na lava iliyotiririka na kuingia baharini.

TAARIFA FUPI

  • Idadi ya watu: Jamhuri ya Ireland ina watu karibu milioni 4.5; na Ireland Kaskazini ina watu karibu milioni 1.8

  • Miji mikuu: Dublin ni mji mkuu wa Jamhuri ya Ireland; Belfast ni mji mkuu wa Ireland Kaskazini

  • Lugha: Kiingereza na Kiireland

  • Hali ya hewa: Joto la wastani na mvua

  • Dini kuu: Ukatoliki katika Jamhuri ya Ireland; na Uprotestanti na Ukatoliki katika Ireland Kaskazini

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki