Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 9/15 kur. 12-13
  • Kutembelea Nikaragua

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutembelea Nikaragua
  • Amkeni!—2015
Amkeni!—2015
g 9/15 kur. 12-13
Ometepe, kisiwa kilichofanyizwa na milima miwili ya volkano katika Ziwa Nikaragua

Kisiwa cha Ometepe kilichopo katika Ziwa la Nikaragua kimefanyizwa na milima miwili ya volkano iliyounganishwa na rasi

NCHI NA WATU

Kutembelea Nikaragua

Ramani ya Nikaragua

MARA nyingi watu huiita Nikaragua nchi yenye maziwa na volkano. Ziwa Nikaragua ndilo ziwa kubwa zaidi katika Amerika ya Kati. Wenyeji wanaliita Cocibolca, neno linalomaanisha “Bahari Tamu.” Ziwa hilo lina mamia ya visiwa na ni ziwa pekee lenye maji baridi lililo na viumbe wa baharini kama vile papa, chuchunge, na tarpon.

Sacuanjoche (frangipani), ua ambalo ni kitambulisho cha taifa la Nikaragua

Ua aina ya sacuanjoche (frangipani) ni mojawapo ya kitambulisho cha taifa la Nikaragua

Nchi ya Nikaragua ina eneo lililo mbali zaidi katika Amerika ya Kati—Pwani ya Mosquito. Pwani hiyo ina upana wa kilomita 65, ulio pembezoni mwa eneo la ufuo upande wa mashariki hadi karibu na nchi jirani ya Honduras. Wamiskito (njia ya nyingine ya kutamka jina Mosquito) ni kabila mojawapo nchini Nikaragua ambalo limekuwapo kabla hata Wazungu kuingia katika nchi hiyo katika karne ya 16.

Wamiskito hupenda kushirikiana na wana desturi za pekee. Kwa mfano, Kimiskito hakina maneno rasmi ya kutambulisha mtu kama vile “Bwana” au “Bibi.” Katika maeneo mengi ya vijijini, vijana huwaita watu waliowazidi umri, “Mjomba” au “Shangazi,” iwe ni ndugu zao au la. Pia, ni desturi ya muda mrefu miongoni mwa Wamiskito kwa mwanamke kumsalimia rafiki wa karibu au ndugu kwa kugusana mashavu. Kisha, mwanamke aliyeanza kutoa salamu huvuta pumzi kupitia pua yake.

Wenyeji wa Nikaragua

Wenyeji wa Nikaragua

Machapisho yanayozungumzia Biblia katika lugha ya Kimayangna na Kimiskito

Machapisho yanayozungumzia Biblia katika lugha ya Kimayangna na Kimiskito, yaliyochapishwa na Mashahidi wa Yehova

TAARIFA FUPI

  • Idadi ya watu: 6,176,000

  • Lugha rasmi: Kihispania. Hata hivyo, katika mikoa iliyojitenga, Kimiskito, Kimayangna, Kirama, na Krioli cha Kiingereza hutumiwa.

  • Serikali: Jamhuri

  • Mji mkuu: Managua

  • Hali ya hewa: Joto kwa kiasi fulani huku kukiwa na baridi maeneo ya milimani

  • Nchi: Pwani iliyo tambarare na maeneo yenye milima

PIMA UJUZI WAKO

Jibu kweli au si kweli kuhusu Nikaragua kwa kutumia sentensi zifuatazo:

  1. Jina la nchi hiyo linatokana na Nicarao, aliyekuwa kiongozi wa kabila moja katika eneo hilo karne nyingi zilizopita.

  2. Nikaragua ni nchi pekee katika Amerika ya Latini iliyotawaliwa na Wahispania na Waingereza.

  3. Katika karne zilizopita, majiji yaliyo katika fuo za Ziwa Nikaragua ilivamiwa na maharamia kutoka visiwa vya Karibea.

  4. Nikaragua ni nchi pekee iliyo na idadi ndogo ya watu katika Amerika ya Kati.

Majibu: Sentensi zote ni za kweli.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki