Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g16 Na. 1 kur. 12-13
  • Kutembelea Liechtenstein

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutembelea Liechtenstein
  • Amkeni!—2016
Amkeni!—2016
g16 Na. 1 kur. 12-13
Daraja nchini Liechtenstein

NCHI NA WATU

Kutembelea Liechtenstein

Ramani ikionyesha jinsi nchi ya Liechtenstein inavyopakana na Uswisi na Austria

LIECHTENSTEIN ni moja kati ya nchi ndogo zaidi duniani. Nchi hiyo iko kwenye milima ya Alps katikati ya Uswisi na Austria. Waselti, Waraetia, Waroma, na Waalemani wamewahi kuishi hapo. Leo, karibu robo tatu ya wakazi wa Liechtenstein ni wazawa wa kabila la Waalemani, ambao wameishi hapo kwa miaka 1,500 hivi.

Lugha kuu inayozungumzwa Liechtenstein ni Kijerumani, hata hivyo lahaja hutofautiana kati ya kijiji kimoja na kingine. Baadhi ya vyakula vya asili ni Tüarka-Rebel, kinachotengezwa kwa kutumia mahindi, na Käsknöpfle, yaani, tambi zenye jibini.

Aina mbili za vyakula vya Liechtenstein

Käsknöpfle

Mwanamke na msichana mdogo nchini Liechtenstein wakiwa wamevaa mavazi ya kienyeji yenye kuvutia

Mavazi ya kitamaduni yenye rangi mbalimbali

Watalii wanapotembelea eneo hilo wao huona milima iliyofunikwa na theluji, mabonde ya kijani, mashamba ya mizabibu, na mimea mbalimbali. Kwa mfano, kuna karibu aina 50 za okidi za msituni katika nchi hiyo ndogo. Pia, kuna majumba ya makumbusho, kumbi za sinema, na viwanda vya kutengeneza divai. Hivyo, watalii hutembelea nchi hiyo kila wakati, iwe kuna majira ya kiangazi au ya baridi kali.

Mashahidi wa Yehova wamekuwapo nchini humo tangu miaka ya 1920. Kwa sasa, kuna Mashahidi 90 hivi nchini humo, wanaowafundisha Biblia wageni na wenyeji.

Kitabu Biblia Inafundisha Nini Hasa? kinachapishwa na Mashahidi wa Yehova katika Kijerumani, lugha kuu ya Liechtenstein, na pia kinapatikana kwenye Intaneti katika www.jw.org.

HABARI FUPI

  • Idadi ya watu: 37,000

  • Mji mkuu: Vaduz

  • Lugha: Kijerumani

  • Dini: Wengi ni Wakatoliki

PIMA UJUZI WAKO

Mambo gani yafuatayo ni sahihi kuhusu Liechtenstein?

  1. Moja kati ya nchi mbili duniani zilizozungukwa na nchi ambazo hazina bandari.

  2. Nchi yenye aina zaidi ya 50 za mamalia.

  3. Nchi yenye aina zaidi ya 1,600 za mimea.

  4. Nchi isiyokuwa na jeshi.

Jibu: Mambo yote manne ni sahihi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki