Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g16 Na. 4 kur. 12-13
  • Kutembelea Kyrgyzstan

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutembelea Kyrgyzstan
  • Amkeni!—2016
Amkeni!—2016
g16 Na. 4 kur. 12-13
Yurts kwenye bonde la Tash Rabat nchini Kyrgyzstan

Nyumba zinazofanana na mahema zinazoitwa Yurts kwenye bonde la Tash Rabat

NCHI NA WATU

Kutembelea Kyrgyzstan

Ramani inayoonyesha nchi ya Kyrgyzstan

NCHI ya Kyrgyzstan ipo Asia ya Kati, imezungukwa na milima mirefu yenye vilele vilivyofunikwa na theluji, na inapakana na nchi za Kazakhstan, Uzbekistan, Tajikistan, na China. Karibu asilimia 90 ya nchi hiyo ni milima. Kyrgyzstan inajivunia kuwa na kilele kirefu cha mlima katika safu ya milima ya Tian Shan ambacho kipo meta 7,439 kutoka usawa wa bahari. Karibu asilimia nne ya nchi hiyo ni misitu. Inasemekana kwamba Kyrgyzstan ndiyo nchi pekee duniani ambapo misitu mikubwa ya miti ya mijozi ya asili inapatikana.

Shahidi wa Yehova akijifunza Biblia na mwanamke wa Kyrgyzstan

Mashahidi wa Yehova wanawafundisha Biblia maelfu ya watu nchini Kyrgyzstan

Watu wa Kyrgyzstan wanajulikana kwa ukarimu na kuwaheshimu wengine. Nchini Kyrgyzstan inafaa kutumia neno “wewe” kwa upole unapomtambulisha mtu aliyekuzidi umri na pia kumpisha aketi kwenye kiti ndani ya usafiri wa umma au kumruhusu aketi kwenye kiti cha mbele wakati wa matukio ya pekee.

Kwa kawaida familia huwa na watoto watatu au zaidi. Mara nyingi mvulana wa mwisho huishi na wazazi wake hata baada ya kuoa ili awatunze watakapozeeka.

Wasichana wanafundishwa kazi mbalimbali za nyumbani ili waweze kutunza familia zao vizuri. Kufikia umri wa utineja, tayari wasichana hao wanakuwa na ustadi wa kutosha wa kutunza familia zao. Kwa kawaida zawadi hutayarishwa kwa ajili ya bibi arusi. Zawadi hizo zinatia ndani matandiko ya kila aina, mavazi mbalimbali na zulia lililotengenezwa kwa mikono. Bwana arusi hutoa pesa na mifugo kama mahari.

Kondoo au farasi huchinjwa wakati wa sherehe au mazishi. Nyama hizo hugawanywa vipande na kila kipande kinakuwa maalumu kwa ajili ya mtu fulani pekee. Kwa kuwa watu hao wanaheshimu sana utamaduni wao, kila mtu hupewa kipande cha nyama kulingana na umri wake, au wadhifa katika jamii. Baada ya ugawaji huo wanakula chakula kikuu cha nchi hiyo kinachoitwa Beshbarmak. Chakula hicho huliwa kwa mikono.

Mwanamume akicheza komuz

Komuz ni kifaa cha muziki kinachojulikana sana

HABARI FUPI

Biblia Inafundisha Nini Hasa?

Kitabu Biblia Inafundisha Nini Hasa? kimechapishwa katika lugha ya Kikirghiz na kinapatikana kwenye intaneti katika www.jw.org

  • Idadi ya watu: 5,776,000

  • Mji mkuu: Bishkek

  • Lugha: Kikirghiz, Kirusi

  • Bidhaa zinazouzwa nje ya nchi: Pamba, sufu, dhahabu, zebaki, urani

  • Dini: Asilimia 80 ya wakazi ni Waislamu

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki