Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g19 Na. 2 kur. 12-13
  • Umuhimu wa Mwongozo wa Watu Wazima

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Umuhimu wa Mwongozo wa Watu Wazima
  • Amkeni!—2019
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • MWONGOZO HUO UNAHUSISHA NINI?
  • KWA NINI MWONGOZO WA WATU WAZIMA NI MUHIMU?
  • JINSI YA KUTOA MWONGOZO
  • Jinsi ya Kutoa Mwongozo Kama Mzazi
    Msaada kwa Ajili ya Familia
  • Kubalehe—Kujitayarisha Kuwa Mtu Mzima
    Amkeni!—2011
  • Mashauri Yenye Kutegemeka Kuhusu Kulea Watoto
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
  • Maswali Ambayo Wazazi Huuliza
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 1
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2019
g19 Na. 2 kur. 12-13
Mwanamke akimwonyesha binti mdogo picha zake za zamani

SOMO LA 5

Umuhimu Wa Mwongozo Wa Watu Wazima

MWONGOZO HUO UNAHUSISHA NINI?

Watoto wanahitaji ushauri na mwongozo kutoka kwa watu wazima. Ukiwa mzazi, una nafasi kubwa ya kutimiza daraka hilo, na kimsingi, hilo ni jukumu lako. Hata hivyo, watu wengine wenye umri mkubwa wanaweza pia kuwashauri na kuwasaidia watoto wako.

KWA NINI MWONGOZO WA WATU WAZIMA NI MUHIMU?

Katika nchi nyingi, vijana hushirikiana mara chache sana na watu wenye umri mkubwa. Hebu fikiria:

  • Watoto hutumia muda mwingi shuleni, mahali ambapo walimu na watu wengine wenye umri mkubwa ni wachache ukilinganisha na idadi ya wanafunzi.

  • Wakitoka shuleni, watoto wengi hukaa wenyewe tu nyumbani kwa sababu wazazi wao wapo kazini.

  • Utafiti fulani ulionyesha kwamba, nchini Marekani, watoto walio na umri kati ya miaka 8 hadi 12 hutumia kwa wastani saa sita kila siku wakicheza michezo ya video, wakitazama televisheni, na kusikiliza muziki.a

Kitabu Hold On to Your Kids kinasema: “Siku hizi vijana hawaigi au kutafuta ushauri na mwongozo kutoka kwa mama, baba, walimu, au watu wengine wenye umri mkubwa, bali kwa . . . vijana wenzao.”

JINSI YA KUTOA MWONGOZO

Tenga wakati wa kuwa na mtoto wako

KANUNI YA BIBLIA: “Mzoeze mtoto njia anayopaswa kuifuata; hata atakapozeeka hataiacha.”​—Methali 22:6, maelezo ya chini.

Kwa kawaida, watoto hutazamia kupata mwongozo kutoka kwa wazazi wao. Isitoshe, wataalamu wanasema kwamba hata watoto wanapoanza kubalehe, bado wao huthamini ushauri wa wazazi wao kuliko wa vijana wenzao. Dakt. Laurence Steinberg aliandika hivi kwenye kitabu You and Your Adolescent: “Vijana walio katika kipindi cha kubalehe hadi wale wanaoanza kuwa watu wazima bado huwa na mwelekeo mkubwa wa kufuata mtazamo na tabia za wazazi wao.” Anaongezea kusema: “Vijana wanaobalehe hupenda kujua unachofikiria na wao husikiliza unachosema, hata ikiwa nyakati nyingine hawakwambii au kukubaliana na maoni yako.”

Mtoto wako ana tamaa ya kupata mwongozo wako, hivyo tumia fursa hiyo vizuri. Tenga wakati wa kuwa naye na umweleze maoni yako, kanuni unazofuata, na mambo uliyopitia maishani.

Mtafutie mtu anayeweza kuwa akimshauri.

KANUNI YA BIBLIA: “Anayetembea na wenye hekima atakuwa na hekima.”​—Methali 13:20.

Je, kuna mtu yeyote mwenye umri mkubwa ambaye ungependa mtoto wako aige mfano wake? Je, unaweza kufanya mipango ili mtu huyo na mtoto wako wapate nafasi za kuwa pamoja? Bila shaka, hilo halimaanishi kwamba utatelekeza jukumu lako ukiwa mzazi. Lakini mtoto wako atanufaika kutokana na mchango wa mtu mwingine mwenye umri mkubwa pamoja na mambo ambayo unamfundisha. Timotheo, anayetajwa kwenye Biblia, alinufaika sana kwa kushirikiana na mtume Paulo hata baada ya kuwa mtu mzima, na Paulo alinufaika kwa kushirikiana na Timotheo.​—Wafilipi 2:20, 22.

Katika miaka 100 iliyopita, familia nyingi zimetawanyika; bibi na babu, wajomba, shangazi, na washiriki wengine wa familia wanaweza kuwa wanaishi nchi tofauti-tofauti. Ikiwa hali ya familia yenu iko hivyo, jitahidi kuandaa fursa za mtoto wako kushirikiana na watu wengine wenye umri mkubwa walio na sifa ambazo ungependa asitawishe.

a Utafiti huo ulionyesha kwamba, vijana wenye umri wa kati ya miaka 13 hadi 19 hutumia kwa wastani karibu saa tisa kila siku wakicheza michezo ya video, wakitazama televisheni, na kusikiliza muziki. Muda unaotajwa kwenye takwimu hizi mbili, hautii ndani muda wanaotumia kwenye mtandao wakiwa shuleni au wakifanya kazi za shule.

Mwanamke akimwonyesha binti mdogo picha zake za zamani

MZOEZE SASA

Kuna uwezekano mkubwa kwamba mtoto anayefuata mwongozo wa watu wazima atakuwa mkomavu na mwenye hekima baadaye

Weka Kielelezo

  • Je, ninawawekea kielelezo kizuri watoto wangu?

  • Je, ninawaonyesha watoto wangu kwamba mimi pia hufuata kielelezo cha wale walio na uzoefu mkubwa zaidi?

  • Je, mimi hutenga wakati wa kuwa na watoto wangu na hivyo kuwaonyesha kwamba ninawathamini?

Mambo Tuliyofanya . . .

“Nyakati fulani, ninapokuwa naendelea na shughuli zangu, binti yangu anaweza kuniambia anataka tuongee. Siku zote mimi huwa tayari kuacha kile ninachofanya ili nimsikilize, hata ikiwa nitahitaji kumwambia anisubiri kwa dakika chache ili nimsikilize kwa makini. Mimi na mke wangu tunajitahidi kuweka kielelezo kizuri ili binti yetu aone tunaishi kupatana na kanuni tunazomfundisha.”​—David.

“Binti yetu alipozaliwa, mimi na mume wangu tuliamua kwamba nitaacha kufanya kazi ili nimlee. Sijutii kufanya uamuzi huo. Ni muhimu sana kuwa karibu na mtoto kadiri anavyokua ili uweze kumpatia ushauri na mwongozo unaofaa. Na si hilo tu, kuwa pamoja naye kunamthibitishia kwamba unamjali.”​—Lisa.

KUSHIRIKIANA NA WATU WAZIMA

“Watoto wangu wamekulia mazingira yenye watu wengi wenye umri mkubwa na ambao wana mitazamo tofauti-tofauti, na hilo limewasaidia kuona mambo kwa upana zaidi. Kwa mfano, walishangaa sana bibi (nyanya) yangu alipowaambia kwamba alipokuwa binti mdogo, familia yao ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata taa ya umeme. Aliwaambia kwamba watu walioishi katika eneo hilo walikuwa wakija kwenye nyumba yao na kusimama jikoni ili waone tu taa ikiwashwa na kuzimwa. Hadithi hiyo iliwasaidia watoto wangu kuona jinsi ambavyo maisha yalikuwa tofauti zamani. Kujifunza mambo kama hayo kuhusu bibi yangu, kuliwachochea wamheshimu na kuwaheshimu watu wengine wenye umri mkubwa. Ikiwa watoto wanashirikiana na watu wenye umri mkubwa kuliko wanavyoshirikiana na vijana wenzao, mtazamo wao wa maisha hubadilika.”​—Maranda.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki