Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ufufuo
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
    • Ufu. 20:13, 14: “Bahari ikawatoa wale wafu waliokuwa ndani yake, na kifo na Kaburi vikawatoa wale wafu waliokuwa ndani yake, nao walihukumiwa kila mmoja kulingana na matendo yake. Na kifo na Kaburi vikatupwa ndani ya lile ziwa la moto. Hili linamaanisha kifo cha pili, lile ziwa la moto.” (Kwa hiyo, wale ambao kifo chao kilitokana na dhambi ya Adamu watafufuliwa, hata kama walizikwa katika bahari au katika Kaburi.)

      Ona pia kichwa “Wokovu.”

      Ikiwa mabilioni ya watu watafufuliwa kutoka kwa wafu, wote wataishi wapi?

      Kadirio la hesabu ya watu ambao wamepata kuishi duniani ni 20,000,000,000. Kama tulivyoona, si wote watakaofufuliwa. Lakini, hata tukisema kwamba wote watafufuliwa, bado kutakuwa na nafasi ya kutosha. Eneo la nchi kavu la dunia sasa ni kama kilometa za mraba 147,600,000. Nusu ya eneo hilo ikitengwa kwa makusudi mengine, bado kutakuwa na eneo la karibu eka moja kwa kila mtu, nalo linaweza kutoa chakula kingi kuliko kile kinachohitajiwa. Chanzo cha upungufu wa chakula leo si kutoweza kwa dunia kuzaa chakula cha kutosha, bali ni ushindani wa kisiasa na pupa ya kibiashara.

      Ona pia ukurasa wa 73, chini ya kichwa “Dunia.”

  • Uhai
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
    • Uhai

      Maana: Hali inayotofautisha mimea, wanyama, wanadamu, na watu wa roho kutoka kwa vitu visivyo na uhai. Vitu hai vinavyoonekana vinaweza kukua, kula, kuhisi, na kuzaana. Mimea ina uhai lakini si uhai kama ule wa nafsi inayoweza kuhisi. Katika nafsi zilizo duniani, wanyama na wanadamu, kuna nguvu za uhai zinazotenda na kuzifanya ziwe hai na pia kuna pumzi inayoendeleza nguvu hizo za uhai.

      Uhai katika maana kamili zaidi, kama ule wa watu wenye akili, ni maisha makamilifu pamoja na haki ya kuwa hai. Nafsi ya wanadamu inaweza kufa. Lakini watumishi waaminifu wa Mungu wana tarajio la kuishi milele wakiwa wakamilifu—wengi wataishi duniani, na washiriki wa “kundi dogo” wataishi mbinguni wakiwa warithi wa Ufalme wa Mungu. Wanapofufuliwa na kuwa viumbe wa roho, washiriki wa jamii ya Ufalme huvikwa kutoweza kufa, uhai usiohitaji kuendelezwa kwa kitu chochote kilichoumbwa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki