Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mbingu
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
    • “Umati mkubwa mbinguni” unaotajwa katika Ufunuo 19:1, 6 si sawa na ule “umati mkubwa” wa Ufunuo 7:9. Wale walio mbinguni hawasemwi kuwa ‘wametoka katika mataifa yote’ wala hawamhesabii Mwana-Kondoo wokovu wao; wao ni malaika. Maneno “umati mkubwa” yanatumiwa katika miktadha katika Biblia.—Marko 5:24; 6:34; 12:37.

      Wale wanaoenda mbinguni watafanya nini huko?

      Ufu. 20:6: “Watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala wakiwa wafalme pamoja naye ile miaka elfu.” (Ona pia Danieli 7:27)

      1 Kor. 6:2: “Hamjui kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu?”

      Ufu. 5:10: “Ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu, nao watatawala wakiwa wafalme juu ya dunia.”

      Ni nani anayewachagua wale watakaoenda mbinguni?

      2 The. 2:13, 14: “Tuna wajibu wa kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, akina ndugu mnaopendwa na Yehova, kwa sababu Mungu aliwachagua ninyi tangu mwanzo kwa ajili ya wokovu kwa kuwatakasa ninyi kwa roho na kwa imani yenu katika kweli. Kwa lengo hili aliwaita ninyi kupitia habari njema tunayoitangaza, kwa kusudi la kujipatia utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.”

      Rom. 9:6, 16: “Si wote wanaotokana na Israeli ni ‘Israeli’ kikweli.   . . . Haitegemei yule anayetaka wala yule anayekimbia, bali hutegemea Mungu, aliye na rehema.”

  • Misa
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
    • Misa

      Maana: Kama inavyoelezwa na Kundi Takatifu la Ibada za Kanisa Katoliki, Misa ni “—Dhabihu ambayo katika hiyo Dhabihu ya Msalaba inadumishwa;—Ukumbusho wa kifo na ufufuo wa Bwana, aliyesema ‘fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu’ (Luka 22:19);—Karamu takatifu ambapo, kupitia ushirika wa Mwili na Damu ya Bwana, Watu wa Mungu hushiriki faida za Dhabihu ya Pasaka, hufanya upya Agano Jipya ambalo Mungu amefanya pamoja na wanadamu mara moja kwa wakati wote kupitia Damu ya Kristo, na katika imani na tumaini hutangulia kuonyesha na kutarajia karamu ya mwisho katika ufalme wa Baba, wakitangaza kifo cha Bwana ‘hata ajapo.’” (Eucharisticum Mysterium, Mei 25, 1967) Hiyo ndiyo njia ya Kanisa Katoliki ya kufanya kile wanachoelewa kwamba Yesu Kristo alifanya katika Mlo wa Jioni wa Bwana.

      Je, mkate na divai vinabadilishwa hakika na kuwa mwili na damu ya Kristo?

      Katika “Ungamo Zito la Imani” Juni 30, 1968, Papa Paulo wa Sita alitangaza hivi: “Tunaamini kwamba kama vile mkate na divai vilivyotakaswa na Bwana katika Mlo wa Jioni wa Bwana vilibadilishwa vikawa Mwili Wake na Damu Yake ambavyo vilipasa kutolewa kwa ajili yetu juu ya msalaba, vivyo hivyo mkate na divai vinavyotakaswa na padri vinabadilishwa na kuwa Mwili na Damu ya Kristo aliyetawazwa kwa utukufu mbinguni, na Sisi tunaamini kwamba kuwapo kwa kifumbo kwa Bwana, chini ya kuonekana kwa vitu hivyo vinavyoonekana kwa hisia zetu kuwa ni vilevile baadaye kama kabla ya Utakaso, ni kuwapo ambako ni kwa kweli na halisi. . . . Kwa kufaa, Kanisa linaliita badiliko hilo la kifumbo kuwa kubadilika kwa mkate na divai kuwa mwili na damu halisi ya Kristo.” (Official Catholic Teachings—Christ Our Lord, Wilmington, N.C.; 1978, Amanda G. Watlington, uku. 411) Je, Maandiko Matakatifu yanakubaliana na imani hiyo?

      Yesu alimaanisha nini aliposema, “Huu ndio mwili wangu,” “Hii ndiyo damu yangu”?

      Mt. 26:26-29, UV: “Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akisema, Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu. Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki, kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.”

      Kuhusu maneno “huu ndio mwili wangu” na “hii ndiyo damu yangu,” kumbuka mambo haya yafuatayo: Mo husema hivi, “huu unamaanisha mwili wangu,” “hii inamaanisha damu yangu.” (Italiki zimeongezwa.) NW husema vivyo hivyo. LEF hutafsiri maneno hayo hivi, “huu unawakilisha mwili wangu,” “hii inawakilisha damu yangu.” (Italiki zimeongezwa.) Tafsiri hizo zinapatana na yale yanayosemwa katika muktadha, katika mstari wa 29, katika chapa mbalimbali za Kikatoliki. VB husema hivi: “Sitakunywa tena mazao haya ya mzabibu, mpaka siku ile nitakapokunywa yale mapya, pamoja nanyi, katika ufalme wa Babangu.” (Italiki zimeongezwa.) UV, ZSB, BHN pia huonyesha Yesu akielekeza kwenye kile kilichokuwa katika kikombe kama “uzao huu wa mzabibu,” “matunda ya mizabibu,” “divai ya zabibu,” na hiyo ilikuwa baada ya Yesu kusema, “Hii ndiyo damu yangu.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki