-
UbatizoKutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
-
-
Luka 3:16, 17: “Yeye [Yesu Kristo] atawabatiza ninyi kwa . . . moto. Sepetu yake ya kupepetea imo mkononi mwake ili kuusafisha kabisa uwanja wake wa kupuria . . . Makapi atayateketeza kwa moto usioweza kuzimwa.” (Uharibifu wa makapi hayo utakuwa wa milele.)
Mt. 13:49, 50: “Hivyo ndivyo itakavyokuwa katika umalizio wa mfumo wa mambo: malaika watatoka kwenda na kuwatenga waovu kutoka katikati ya waadilifu nao watawatupa ndani ya tanuru ya moto.”
Luka 17:29, 30: “Siku ambayo Loti alitoka Sodoma kulinyesha moto na kiberiti kutoka mbinguni na kuwaangamiza wote. Itakuwa vivyo hivyo siku ile ambayo Mwana wa binadamu atafunuliwa.”
Si sawa na ubatizo kwa roho takatifu, uliokuwa wa wanafunzi
Mdo. 1:5: “Yohana, kwa kweli, alibatiza kwa maji, lakini ninyi [mitume waaminifu wa Yesu] mtabatizwa kwa roho takatifu siku chache baadaye.”
Mdo. 2:2-4: “Ghafula kukatokea kutoka mbinguni kelele kama ile ya upepo wenye nguvu unaovuma, nao ukaijaza nyumba yote ambamo walikuwa wameketi. Nao wakaona ndimi kama za moto, nazo zikagawanyika huku na huku, na mmoja ukaketi juu ya [lakini haukumfunika au kumzamisha] kila mmoja wao, nao wote wakajazwa roho takatifu wakaanza kusema katika lugha tofauti, kama vile roho ilivyokuwa ikiwawezesha kusema.”
-
-
UfalmeKutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
-
-
Ufalme
Maana: Ufalme wa Mungu huwakilisha enzi kuu ya Yehova ya ulimwengu wote kuelekea viumbe wake, au njia anayoitumia kuonyesha enzi hiyo. Neno hili linatumiwa hasa kurejelea enzi kuu ya Mungu kupitia serikali inayoongozwa na Mwana wake, Yesu Kristo. Neno “ufalme” linaweza kurejelea utawala wa yule aliyetiwa mafuta awe Mfalme, au linaweza kurejelea dunia inayotawaliwa na serikali hiyo ya mbinguni.
Je, Ufalme wa Mungu ni serikali halisi?
Au ni hali iliyo katika mioyo ya wanadamu?
Luka 17:21, UV: “Wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama ufalme wa Mungu umo ndani yenu [pia ZSB, NAJ; lakini “kati yenu,” BHN, VB; “katikati yenu,” NW].” (Ona kwamba, kama vile mstari wa 20 unavyoonyesha, Yesu alikuwa akizungumza na Mafarisayo, ambao pia aliwashutumu kuwa wanafiki, kwa hiyo, hangeweza kumaanisha kwamba Ufalme ulikuwa katika mioyo yao. Lakini Ufalme kama unavyowakilishwa na Kristo ulikuwa katikati yao.)
-