Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Uponyaji
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
    • Maadamu mtu ameponywa, jinsi uponyaji huo hufanywa ni muhimu kweli?

      2 The. 2:9, 10: “Kuwapo kwa huyo mwasi-sheria ni kulingana na utendaji wa Shetani pamoja na kila tendo lenye nguvu [“kila namna ya miujiza,” BHN] na ishara za uwongo na mambo ya ajabu na pamoja na kila udanganyifu usio wa uadilifu kwa wale wanaoangamia, kuwa malipo kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli ili wapate kuokolewa.”

      Luka 9:24, 25: “Yeyote yule anayetaka kuiokoa nafsi [“maisha,” BHN] yake ataipoteza; lakini yeyote yule anayeipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeiokoa. Kwa kweli, mtu anapata faida gani ikiwa anaupata ulimwengu wote lakini aipoteze nafsi yake mwenyewe au apate hasara?”

      Kuna tumaini gani la kuponywa kikweli magonjwa yote?

      Ufu. 21:1-4: “Nikaona mbingu mpya na dunia mpya; kwa maana mbingu ya kwanza na dunia ya kwanza zilikuwa zimepitilia mbali . . . ‘Naye [Mungu] atafuta kila chozi kutoka katika macho yao, na kifo hakitakuwapo tena, wala maombolezo wala kilio wala maumivu hayatakuwapo tena. Mambo ya zamani yamepitilia mbali.’”

      Isa. 25:8: “Kwa kweli atameza kifo milele, na Bwana Mwenye Enzi Kuu Yehova hakika atafuta machozi katika nyuso zote.” (Pia Ufunuo 22:1, 2)

      Isa. 33:24: “Hakuna mkaaji atakayesema: ‘Mimi ni mgonjwa.’”

      Mtu Akisema—

      ‘Je, unaamini uponyaji?’

      Unaweza kujibu hivi: ‘Yeyote ambaye haamini kwamba Mungu ana uwezo wa kuponya haiamini Biblia. Lakini nina shaka ikiwa watu wanafanya uponyaji kwa njia iliyo sawa leo.’ Kisha unaweza kuongezea: (1) ‘Acha nikusomee andiko moja, na uone ikiwa unatambua zoea lililo tofauti sana leo. (Mt. 10:7, 8) . . . Je, unatambua pia jambo fulani hapa ambalo Yesu alisema wanafunzi wake wangeweza kufanya lakini ambalo waponyaji wa leo wameshindwa kulifanya? (Hawawezi kufufua wafu.)’ (2) ‘Sisi hatuwahukumu watu wengine, lakini ona kwamba andiko la Mathayo 24:24 linataja jambo fulani tunalohitaji kujihadhari nalo.’

      Au unaweza kusema: ‘Ninaamini hakika kwamba yale ambayo Biblia inasema kuhusu uponyaji ni ya kweli. Lakini uponyaji wowote unaofanywa katika mfumo huu wa mambo ni wa faida za muda mfupi tu, sivyo? Mwishowe sisi sote hufa. Je, kutakuwa na wakati ambapo kila mtu anayeishi atakuwa na afya njema naye hatakufa kamwe? (Ufu. 21:3, 4)’

  • Urithi wa Upapa
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
    • Urithi wa Upapa

      Maana: Fundisho la kwamba wale mitume 12 wana warithi ambao wamepokea mamlaka iliyopitishwa kutoka kwa Mungu. Katika Kanisa Katoliki, inasemekana kwamba maaskofu wakiwa kikundi ni warithi wa mitume, na papa anadaiwa kuwa mrithi wa Petro. Inaaminiwa kwamba mapapa Wakatoliki wanamfuata Petro, ambaye inasemwa kwamba Kristo alimpa ukuu wa mamlaka juu ya Kanisa zima, wakichukua cheo cha Petro na kutimiza kazi zake. Hilo si fundisho la Biblia.

      Je, Petro ndiye “mwamba” ambao kanisa lilijengwa juu yake?

      Mt. 16:18, UV: “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.” (Katika muktadha [mstari wa 13 na wa 20], ona kwamba mazungumzo hayo yanakazia utambulisho wa Yesu.)

      Mitume Petro na Paulo walielewa nani kuwa “mwamba,” lile “jiwe la pembeni”?

      Mdo. 4:8-11, UV: “Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee . . . kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu. Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni.”

      1 Pet. 2:4-8, UV: “Mmwendee yeye [Bwana Yesu Kristo], . . . ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo. Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, na kila amwaminiye hatatahayarika. Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, jiwe walilolikataa waashi, limekuwa jiwe kuu la pembeni. Tena, jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki