Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w10 5/1 uku. 3
  • Mungu Yuko Wapi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mungu Yuko Wapi?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Habari Zinazolingana
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2006
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2005
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2003
  • Ni Nini Husababisha Ukosefu wa Makao?
    Amkeni!—2005
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
w10 5/1 uku. 3

Mungu Yuko Wapi?

Septemba 11, 2001 (11/9/2001): Mwendo wa saa 2 na dakika 46 asubuhi, ndege ya abiria inagonga jengo la kaskazini la World Trade Center huko New York City, huo ndio mwanzo wa mashambulizi ya kigaidi yaliyopangwa. Kwa dakika 102 zinazofuata, watu 3,000 hivi wanakufa.

Desemba 26, 2004 (26/12/2004)

Tetemeko la nchi lenye kipimo cha 9.0 katika Bahari ya Hindi linasababisha mawimbi makubwa yenye kuua ambayo yanapiga nchi 11, kutia ndani Afrika, umbali wa kilomita 5,000 hivi. Kwa siku moja tu, watu 150,000 wanakufa au kupotea, na zaidi ya milioni moja wanaachwa bila makao.

Agosti 1, 2009 (1/8/2009): Mwanamume mwenye umri wa miaka 42 pamoja na mwanawe wa miaka 5 wanagonga ukuta wa mbao wa bandari wakiwa ndani ya kigari kinachoteleza juu ya barafu. Baba anakufa. Mwanawe anabaki hai lakini anakufa siku inayofuata. Mtu mmoja wa ukoo aliyefadhaika alisema hivi: “Tulitumaini kwamba kungekuwa na muujiza na kijana huyo angepona.”

Unaposoma kuhusu mashambulizi ya kigaidi au misiba ya asili au unapopatwa na msiba, je, unajiuliza ikiwa Mungu anaona yale yanayotukia? Je, unajiuliza ikiwa ametuacha? Biblia inatoa jibu lenye kufariji, kama tutakavyoona.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]

© Dieter Telemans/Panos Pictures

PRAKASH SINGH/AFP/Getty Images

© Dieter Telemans/Panos Pictures

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki