Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • wp16 Na. 3 uku. 3
  • Mtu Unayempenda Anapokufa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mtu Unayempenda Anapokufa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2016
  • Habari Zinazolingana
  • Wengine Waweza Kusaidiaje?
    Mtu Fulani Umpendaye Anapokufa
  • “Lieni Pamoja na Watu Wanaolia”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2017
  • Naweza Kuishije Nikiwa na Huzuni Yangu?
    Mtu Fulani Umpendaye Anapokufa
  • Jinsi ya Kukabiliana na Huzuni ya Kufiwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2016
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2016
wp16 Na. 3 uku. 3
Mwanamke mwenye huzuni

HABARI KUU

Mtu Unayempenda Anapokufa

“Mwanangu,. . . usilie. Kazi ya Mungu haina makosa.”

Mwanamke anayeitwa Bebe aliambiwa maneno hayo, siku ya mazishi ya baba yake aliyekufa kutokana na aksidenti ya gari.

Bebe alimpenda sana baba yake. Maneno hayo aliyoambiwa na rafiki wa familia mwenye nia nzuri, yalimuumiza sana badala ya kumfariji. Bebe aliendelea kujiambia, “baba hakupaswa kufa.” Kuonyesha kwamba bado alikuwa na huzuni, miaka mingi baadaye Bebe alisimulia tukio hilo katika kitabu chake.

Sawa na Bebe, wengi wanakubali kwamba huzuni ya kufiwa haiishi haraka, hasa ikiwa aliyekufa alikuwa mtu wa karibu sana. Biblia inasema kifo ni “adui wa mwisho.” (1 Wakorintho 15:26) Kifo huharibu maisha yetu na hakizuiliki. Hakuna yeyote kati yenu anayeweza kuepuka madhara ya kifo. Hivyo, haishangazi kwamba tunapopatwa na msiba mara nyingi tunashindwa kukabiliana na hali hiyo.

Huenda ukajiuliza: ‘Huzuni ya kufiwa huisha baada ya muda gani? Mtu anawezaje kukabiliana na huzuni hiyo? Ninaweza kuwafariji jinsi gani wale waliofiwa? Je, kuna tumaini lolote kwa wapendwa wetu waliokufa?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki