Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • wp24 Na. 1 uku. 3
  • Mema na Mabaya: Swali Linalotukabili Sote

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mema na Mabaya: Swali Linalotukabili Sote
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2024
  • Habari Zinazolingana
  • Onyesha Imani​—Amua kwa Hekima!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2017
  • Fanya Maamuzi Ambayo Yanamletea Mungu Heshima
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Jinsi ya Kufanya Maamuzi Mazuri
    Furahia Maisha Milele!—Masomo ya Kujifunza Biblia
  • Utangulizi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2024
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2024
wp24 Na. 1 uku. 3
Kijana aliyekuwa kwenye picha ya awali anasaidiwa na askari wa hifadhi. Anatumia ramani kumwonyesha njia itakayomfikisha anapokwenda, juu ya mlima.

Mema na Mabaya: Swali Linalotukabili Sote

Utafanya nini ikiwa unataka kutembelea sehemu ambayo haujawahi kufika?

  1. 1. Utaelekea upande unaofikiri unapaswa kwenda.

  2. 2. Utawafuata wengine ukitumaini kwamba wanaijua njia.

  3. 3. Utaomba mwongozo kutoka kwenye chanzo kinachotegemeka, kama vile GPS, ramani, au rafiki unayemwamini anayeifahamu njia.

Tukichagua njia ya kwanza au ya pili tunaweza kufika sehemu fulani lakini huenda tusifike mahali tunapoenda. Hata hivyo, tukichagua njia ya tatu, bila shaka tutafika tunapoenda.

Maisha ni safari—na tunatamani safari hii iwe yenye furaha sasa na wakati ujao. Mahali tunapotafuta ushauri tunapofanya maamuzi, pataamua ikiwa safari yetu itafanikiwa au la.

Ingawa maamuzi mengi tunayofanya ni madogo na huenda yasituathiri kwa muda mrefu, maamuzi mengine ni muhimu na yanatuathiri sana maishani. Maamuzi hayo yanaonyesha waziwazi maadili yetu, yaani, maoni yetu kuhusu mema na mabaya. Maamuzi hayo yatatuathiri sisi na wapendwa wetu kwa muda mrefu. Matokeo yanaweza kuwa mazuri au mabaya. Maamuzi hayo ni kuhusu mambo kama vile:

  • Ngono na ndoa

  • Unyoofu, kazi, na pesa

  • Jinsi ya kulea watoto

  • Jinsi ya kuwatendea wengine

Unawezaje kuwa na uhakika kwamba maamuzi yako yatakuletea furaha wewe na familia yako sasa na wakati ujao?

Swali linalotukabili sote ni hili: Ni nini kitakachoongoza maamuzi ninayofanya kuhusu maadili?

Gazeti hili litaelezea kwa nini tunaweza kuamini mambo ambayo Biblia inasema kuhusu mema na mbaya.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki