Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • yb14 kur. 112-113
  • Vikundi vya Siri

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Vikundi vya Siri
  • 2014 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
2014 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
yb14 kur. 112-113

SIERRA LEONE AND GUINEA

Vikundi vya Siri

VIKUNDI vya siri vinapatikana kila mahali katika nchi za Afrika Magharibi na washiriki wake ni watu wa makabila, tamaduni, na lugha mbalimbali. Vikundi hivyo vinaratibu shughuli za kijamii, kielimu, na kisiasa za washiriki wao. Hata hivyo, lengo lao kuu ni dini. Vikundi vikubwa zaidi kuliko vingine vyote ni Poro (kwa ajili ya wanaume) na Sande (kwa ajili ya wanawake).a Kwa mfano, kikundi cha Poro kinahangakia sana “kudhibiti roho waovu na kuhakikisha kwamba roho hao wanapojihusisha katika masuala ya wanaume, inakuwa ni kwa manufaa ya wanaume hao.”​—Initiation, 1986.

Washiriki wapya wa kikundi cha Poro wanafundishwa kuhusu siri za ulimwengu wa roho na nguvu za uchawi, na kufanya tambiko la kuwaweka chale mwilini. Washiriki wapya wa kikundi cha Sande pia wanajifunza kuhusu ulimwengu wa roho na kwa kawaida wanawake hao hukeketwa, ingawa katika baadhi ya maeneo wameacha kukeketa.

Vikundi vingine vya siri vinadhibiti mwenendo wa kingono na kutibu ugonjwa wa akili na magonjwa mengine kwa kutumia dawa za waganga wa kienyeji. Wakati wa vita vya wenywewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone, kikundi kimoja cha siri kilidai kwamba washiriki wake hawawezi kuuawa kwa risasi. Haikuwa kweli.

Washiriki wanakatazwa kabisa kufichua maarifa na taratibu za kikundi. Mtu anayekiuka sheria na masharti ya kikundi cha siri anajihatarisha, kwani adhabu yake ni kifo.

a Katika maeneo fulani, kikundi cha Sande kinajulikana pia kama Bondo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki