Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • yb17 kur. 84-88
  • Maelezo Mafupi Kuhusu Nchi ya Georgia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maelezo Mafupi Kuhusu Nchi ya Georgia
  • 2017 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
2017 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
yb17 kur. 84-88
Kijiji fulani katika eneo la juu la Svaneti nchini Georgia

Eneo la juu la Svaneti

GEORGIA

Maelezo Mafupi Kuhusu Nchi ya Georgia

Mwanamume akiwa amebeba kikapu cha zabibu; vishada vya zabibu

Kuvuna zabibu huleta shangwe kubwa

Nchi Georgia inajulikana kwa safu ya milima na vilele vyenye theluji, vingine vikiwa na urefu wa mita zaidi ya 4,500. Nchi hiyo imegawanywa katika sehemu mbili kuu, sehemu ya mashariki na ya magharibi, kila moja ikiwa na maeneo kadhaa yenye hali ya hewa, tamaduni, muziki, dansi, na chakula cha aina yake.

Watu Wengi wa wakazi wapatao milioni 3.7 ni Wageorgia.

Dini Idadi kubwa ya watu ni Waothodoksi. Asilimia 10 hivi ni Waislamu.

Lugha Kigeorgia hakihusiani na lugha yoyote ya nchi jirani. Historia inaonyesha kwamba alfabeti za pekee za Kigeorgia zilibuniwa Kabla ya Wakati wa Kawaida.

Kazi Watu wengi hujitegemeza kupitia ukulima. Hivi karibuni, utalii umechangia pakubwa katika ukuzi wa uchumi nchini Georgia.

Hali ya hewa Sehemu ya mashariki ya nchi hiyo huwa na hali nzuri ya hewa. Eneo la pwani la Bahari Nyeusi, lililo magharibi mwa Georgia, huwa na hali nzuri ya hewa, na matunda ya jamii ya machungwa hukua kwa wingi.

Watu wakivuna zabibu

Kuvuna zabibu katika eneo la Kakheti

Chakula Kwenye kila mlo wa Mgeorgia, lazima kuwe na mkate. Mkate wa kitamaduni huokwa katika jiko la udongo. Chakula cha kawaida huwa mchuzi mzito wenye vikolezo na viungo vilivyotolewa moja kwa moja kutoka shambani. Divai imetengenezwa nchini Georgia kwa muda mrefu. Katika utamaduni wao, divai huchachishwa na kuwekwa kwenye vyombo vikubwa vya udongo. Familia nyingi hukuza zabibu na kujitengenezea divai. Nchini Georgia, kuna aina 500 hivi za zabibu za kienyeji.

Mwanamke akioka mkate

Kuoka mkate wa kitamaduni

UKUBWA WA NCHI (kilomita za mraba)

26,900

IDADI YA WATU

3,720,400

IDADI YA WAHUBIRI MWAKA 2016

18,619

UWIANO, MHUBIRI 1 KWA

200

HUDHURIO LA UKUMBUSHO MWAKA 2016

32,216

Ramani ya Georgia
    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki