Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • yb17 kur. 169-170
  • Wakurdi Waikubali Kweli

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wakurdi Waikubali Kweli
  • 2017 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
2017 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
yb17 kur. 169-170
Dada akijifunza na mwanamke katika lugha ya Kikurdi

GEORGIA

Wakurdi Waikubali Kweli

“MIMI humshukuru Yehova mara nyingi sana kwamba nilijifunza kumhusu katika lugha yangu ya mama,” anasema Gulizar.

Kwa miaka minane, Gulizar alikuwa mhubiri ambaye hajabatizwa. Alibatizwa baada ya kuhudhuria mikutano katika lugha yake ya Kikurdi. Yeye ni miongoni mwa Wakurdi wengi ambao wamekubali kweli katika miaka ya karibuni nchini Georgia. Wakurdi ni nani?

Wakurdi wameishi katika eneo la Mashariki ya Kati kwa karne nyingi. Wasomi fulani wanafikiri kuwa Wakurdi wametokana na Wamedi wa kale wanaotajwa katika Biblia. (2 Fal. 18:11; Mdo. 2:9) Lugha yao ni mojawapo ya lugha za Iran.

Leo, mamilioni ya Wakurdi wanaishi katika nchi mbalimbali, kutia ndani Armenia, Iraki, Iran, Siria, na Uturuki. Kuna Wakurdi 20,000 hivi nchini Georgia. Kwa ujumla, wao ni watu wanaomwogopa Mungu na wanaheshimu sana mambo ya kiroho.

Sasa nchini Georgia, kuna wahubiri 500 ambao ni Wakurdi na makutaniko matatu ya Kikurdi. Katika mwaka wa 2014, walifurahia sana kusanyiko la eneo la kwanza la Kikurdi jijini Tbilisi, lililokuwa na wajumbe kutoka Armenia, Ujerumani, Ukrania, na Uturuki.

Watoto wa Kikurdi wakifurahia kutazama video za Caleb na Sofia
    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki