Watchtower—MAKTABA KU ENTERNETE
Watchtower
MAKTABA KU ENTERNETE
Kiswahili (Congo)
  • BIBLIA
  • VICHAPO
  • MIKUTANO
  • km 8/96 uku. 5-6
  • Kujikumbusha kwa Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Hakuna video juu ya habari yenye umechagua.

Pole, kulikuwa kosa fulani wakati video ilikuwa inajaribu kusoma.

  • Kujikumbusha kwa Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1996
Huduma Yetu ya Ufalme—1996
km 8/96 uku. 5-6

Kujikumbusha kwa Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Kujikumbusha vitabu vikiwa vyenye kufungwa kwa mambo yaliyofunzwa kwenye Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma toka Mei 6 mpaka Agosti 19, 1996.

[Agizo: Wakati wa kujikumbusha, tumia tu Biblia. Mitajo inayotolewa kisha kila ulizo inatolewa ili kurahisisha utafiti wako mwenyewe. Namba za kurasa na mafungu hazionyeshwi kila mara kuhusu mitajo ya Mnara wa Mlinzi.

Jibu Kweli au Si Kweli kisha maneno yafuatayo:

1. Iwe inawezekana sisi kutoa vitu vingi au vidogo, Maandiko yanatutia moyo kuomba kwa kusisitiza pendeleo la kuwasaidia ndugu zenu Wakristo waaminifu wanaokosa mahitaji ya lazima kwa maisha. (2 Kor. 8:1-4) [jv uku. 314 fu. 1]

2. ‘Gogi wa Magogi’ ni mtajo wa mfano wa serikali za ulimwengu huu. (Ezek. 38:2) [Usomaji wa Biblia; ona wSW91 8/15 uku. 27 fu. 2.]

3. Kama vile Ohola alivyokuwa dada mzaliwa wa kwanza wa Oholiba, kulingana na maelezo ya Ezekieli sura 23, Kanisa katoliki ni dada mzaliwa wa kwanza wa uprotestanti, na matengenezo hayo mawili yalijichafua kwa kufanya uzinifu wa kiroho pamoja na mamlaka ya kibiashara na ya kisiasa ya ulimwengu. [Usomaji wa Biblia; ona wSW89 4/1 uku. 30.]

4. Hesabu ya Mashahidi wa Yehova iliongezeka sana hivi kwamba inakuwa ya juu kuliko raia wa nchi nyingi. [jv uku. 278 fu. 3]

5. Kornelio alikuwa ndiye mtu wa kwanza mtaifa kuwa Mkristo. [ad uku. 336 fu. 10 mpaka uku. 337 fu. 1]

6. Tunaweza kufanya ulinganifu kati ya Yakobo 4:17 na Ezekieli 33:​7-9. Maandiko hayo yanaonyesha kwamba ni ujuzi wa yale Mungu anayotuomba ndio unaotokeza madaraka. [Usomaji wa Biblia; ona wSW93 4/1 uku. 7 fu. 1.]

7. Danieli alijionyesha kuwa nabii wa kweli kwa kufasiria maana ya sanamu iliyoonwa katika ndoto, baada ya mfalme Nebukadneza kumfasiria yenyewe. [Usomaji wa Biblia; ona Danieli 2:7-9, 26.]

8. Maji yaliyokuwa yakitiririka kutoka hekalu ambayo ono linaelezwa katika Ezekieli 47:1 yanamaanisha uwezo unaosafisha wa ubatizo. [Usomaji wa Biblia; ona wSW88 9/15 uku. 27 fu. 20.]

9. Mfano wa Balaamu ni onyo kwa wote wanaofanya ugumu wa shingo na wanaoendelea kutojali mapenzi ya Mungu huku wakitafuta faida yao ya kichoyo. (Yuda 11) [ad uku. 166 fu. 3]

10. Mwandishi mwaminifu wa nabii Yeremia aliyepokea ahadi ya kulindwa salama wakati wa mazingiwa na uharibifu wa Yerusalemu alikuwa Ebedi-Meleki. [ad uku. 175 fu. 10]

Jibu maulizo yafuatayo:

11. Jinsi gani Charles Russell alionyesha kwamba alikuwa akizingatia moyoni kitia-moyo cha Yesu cha kutafuta kwanza Ufalme? (Mt. 6:33) [jv uku. 284 fu. 1]

12. Makusanyiko ya Mashahidi wa Yehova yanashuhudia nini kwa namna isiyobishika? [jv uku. 254 maf. 2, 3]

13. Ni katika maana gani Mashahidi wapakaliwa wa Yehova na wale wanaojiunga nao wanapaswa kuwa kama Ezekieli? (Ezek. 11:25) [Usomaji wa Biblia; ona wSW88 9/15 kur. 16-17 fu. 3.]

14. Kwa nini vikundi vikundi vyenye kutengana vya vijana katika makutaniko vilikomeshwa katika 1938? [jv uku. 246 fu. 2]

15. Ni katika nini malkiya Athalia alimwiga mama yake, Yezebeli? [ad uku. 143 fu. 3]

16. Ni nini maana ya jina la kimungu, Yehova? [klSW uku. 25 fu. 7]

17. Mkristo wa kweli anapopatikana katika uhitaji, ni nani aliye na wajibu wa kwanza wa kumtolea msaada wa kimwili, na ni andiko gani la Biblia linalotegemeza jibu lako? [jv uku. 305 fu. 1]

18. Nani aliyechukua nafasi ya Naomi katika ndoa ya kupiana pamoja na Boazi? [ad uku. 1061 fu. 14]

19. Ni nabii gani alisema juu ya dunia kuwa ni “duara” (mviringo), na ni wapi tunapata wazo hilo katika Maandiko? [klSW uku. 17 fu. 14]

20. Nini linamaanisha kwelikweli kutafuta kwanza Ufalme? [jv uku. 295 fu. 2]

Jaza nafasi zilizo wazi katika misemwa ifuatayo:

21. Katika utimizo wa Ezekieli 21:​26, ufalme “uliyoinuka” wa _____________________ ‘ulishushwa’ kwa kupatwa na uharibifu katika _________________________ , na falme za_________________________ zilizokuwa “chini” ziliweza ‘kuinuliwa,’ kwani tangu hapo ziliweza kutawala dunia bila kusumbuliwa na _________________________ wa Mungu wa mfano. [Usomaji wa Biblia; ona wSW88 9/15 kur. 19-20 fu. 16.]

22. Sehemu moja ya kitabu cha _________________________ kwa wazi ni _________________________ iliyoandikwa mapema; kinatoa uangalifu wacho juu ya ugomvi kati ya nasaba (ukoo) kuu za kifalme muda wa karne nyingi. [siSW uku. 138 fu. 1]

23. Usemi “mtumishi wangu Daudi” unaopatikana katika Ezekieli 34:23 uliandikwa mapema kisha kifo cha _______________ ; unahusu tangazo la kiunabii linalomtaja ________________________ . [siSW uku. 137 fu. 31]     

24. Kati ya Januari 1946 na Agosti 1948, watumishi wa Yehova walituma ________________________ na ________________________ kwa Mashahidi waliotawanyika katika yapata hivi nchi 18 zilizoguswa na _________________________ . [jv uku. 308 fu. 3, 4]

25. Misingi iliweza kuwekwa katika ukuzi wa kiroho katika mwaka 1931 wakati tulipochukua jina la _________________________ , katika 1935 wakati _________________________ ulipotambuliwa, katika 1950 wakati wa kutolewa kwa _________________________  na katika 1962 wakati tuliporekebisha uelewevu wetu wa wale _________________________ . [jv uku. 260 fu. 3 mpaka uku. 264 fu. 2]

Chagua jibu lililo sahihi katika misemwa inayofuata:

26. Yale yaliyomfikia (Abigaili; Dorkasi; Dina) yanayoonyesha vema uhakika wa kanuni inayopatikana katika 1 Wakorinto 15:33. [ad uku. 401 fu. 2]

27. Koreshi aliuvamia mji wa (Yerusalemu; Babiloni; Ninawi) kwa kugeuzia upande mwingine maji (ya Tiro; Yordani; Frati) ili kwamba majeshi yake yaweze kuingia katika mji. [ad uku. 355 fu. 1]

28. Jina lake lilikuwa ni Yusufu, lakini kwa kuwa alikuwa mwenye shauku na mkarimu akaja kujulikana kwa jina la (Andrea; Barnabasi; Batholomayo), jina linalomaanisha “Mwana wa (huzuni; shangwe; faraja).” [ad uku. 174 maf. 7, 8]

29. Belshaza, mwana mzaliwa wa kwanza wa (Koreshi; Nabonido; Nebukadneza), anatajwa katika habari ya Biblia tu na (Ezekieli; Danieli; Isaya), na shuhuda za uchimbuaji wa mambo ya kale unahakikisha kihistoria habari hiyo. [ad uku. 186 fu. 5]

30. Kuanguka kwa Babiloni kulitabiriwa na (Danieli na Hosea; Yoeli na Amosi; Isaya na Yeremia). [klSW uku. 18 fu. 17]

Patanisha Maandiko yafuatayo na misemwa inayolingana nayo:

2 Sik. 14:2-5; Zab. 78:40, 41; Is. 55:10, 11; Dan. 1:8, 11-13; 1 Kor. 9:16.

31. Ili kukazia umuhimu wa kazi ya kuhubiri, Mnara wa Mlinzi ulisema, katika 1950: “Yehova alifanya mahubiri kuwa kazi ya muhimu zaidi ambayo haijapata kutimizwe na yeyote wetu katika ulimwengu huu.” [jv uku. 292 fu. 5]

32. Vijana Wakristo hawangepaswa kusita kuwajulisha kwa heshima wakuu wenye mamlaka na wanashule wenzao kwamba hawatavunja dhamiri yao iliyofunzwa na Mungu. [Usomaji wa Biblia; ona wSW92 11/1 uku. 14 fu. 17.]

33. Kusudi la Mungu la mwanzoni kuelekea wanadamu na dunia litatimia. [klSW uku. 9 fu. 10]

34. Watumishi waaminifu wa Yehova wanapinga kwa uhodari uasi-imani na wanajishughulisha kwa bidii kutetea ibada ya kweli. [ad uku. 128 maf. 6, 7]

35. Mungu ana hisia-moyo, na uchaguzi wetu mbalimbali ni wenye maana machoni pake. [klSW uku. 14 fu. 8]

S-97-SW  #289a 8/96

    Vichapo vya Swahili (Congo) (1996-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili (Congo)
    • Tumia Wengine
    • Préférences
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Kanuni za Matumizi
    • Kanuni za Kutunza Siri
    • Paramètres Kuhusu Kutunza Siri
    • JW.ORG
    • Ingia
    Tumia Wengine