Watchtower—MAKTABA KU ENTERNETE
Watchtower
MAKTABA KU ENTERNETE
Kiswahili (Congo)
  • BIBLIA
  • VICHAPO
  • MIKUTANO
  • km 12/96 uku. 3-4
  • Kujikumbusha Kwa Kuandika Kwa Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Hakuna video juu ya habari yenye umechagua.

Pole, kulikuwa kosa fulani wakati video ilikuwa inajaribu kusoma.

  • Kujikumbusha Kwa Kuandika Kwa Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1996
Huduma Yetu ya Ufalme—1996
km 12/96 uku. 3-4

Kujikumbusha Kwa Kuandika Kwa Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Kujikumbusha vitabu vikiwa vyenye kufungwa kwa mambo yaliyozungumzwa kwenye Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma toka Septemba 2 mpaka lile la Desemba 23, 1996. Jibu kwa kutumia karatasi tofauti kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.

[Agizo: Wakati wa kujikumbusha, tumia tu Biblia. Mitajo inayotolewa kisha kila ulizo inatolewa ili kurahisisha utafiti wako mwenyewe. Namba za kurasa na mafungu hazionyeshwi kila mara kuhusu mitajo ya Mnara wa Mlinzi.]

Jibu Kweli au Si Kweli kisha sentensi zifuatazo:

1. Kama Mariamu mtu wa ukoo wake, Elizabeti alikuwa wa kabila la Yuda. [ad uku. 445 fu. 5]

2. Hakuna “samaki mkubwa” ambaye anaweza hakika kumeza mtu mzima. (Yona 1:17) [siSW uku. 153 fu. 4]

3. Epafrazi na Epafrodito walikuwa wote wawili wenzi-washiriki wa mtume Paulo. [ad uku. 461 fu. 7-8]

4. Unabii wa Danieli 9:​24, 25 unahusu kuzaliwa kwa Yesu. [klSW uku. 36 fu. 8]

5. Ebed-Meleki, tohashi Mwetiopia, alimsaidia Yeremia kutoka ndani ya shimo la matope la Melkiya. [ad uku. 417 fu. 3]

6. Henoko hakufariki kwa kuwa alitwaliwa juu mbinguni pamoja na mwili wake wa nyuma. (Mwan. 5:24) [ad uku. 657 fu. 8]

7. Unabii wa Hosea ulitolewa hasa kwa makabila mawili ya ufalme wa Yuda. [siSW uku. 144 fu. 8]

8. Takwa la kwanza linaloombwa ili kutumikia katika halmashauri ya ujenzi wa jimbo ni kuwa na ujuzi mwingi na maarifa bora katika ujenzi. [jv uku. 325 fu. 6]

9. Kulingana na Sefania 3:​9, watumishi wa Mungu wataungana katika ulimwengu mpya kwa kuwa watasema lugha moja: Kiebrania. [Usomaji wa Biblia; ona wSW89 6/1 uku. 30.]

10. Ni kwa kumtetea Ayubu kwamba Elihu alijionyesha kuwa rafiki wa kweli. [ad uku. 444 maf. 9-10]

Jibu maulizo yafuatayo:

11. Kwa nini ni jambo linalofaa kwamba mahali maalumu pa mkutano wa makutaniko ya ulimwenguni pote papate kuitwa Majumba ya Ufalme, na wapi jengo la kwanza kupata jina hilo lilipatikana? [jv uku. 319 fu. 2]

12. Ni tangazo gani la kibiblia lililofanywa na Waebrania watatu linalofunua kwamba utii wao kwa Mungu haukutokana na ulinzi au wokovu wa kimungu? (Dan. 3:​16-18) [siSW uku. 141 fu. 19]

13. Ni andiko gani lililotangaza mahali pa kuzawaliwa Masiya? [siSW uku. 156 fu. 6]

14. Kwa nini matendo ya uwezo yanayotimizwa kwa jina la Yesu sio ushuhuda hakika wa neema na tegemezo la Mungu? [klSW uku. 46 maf. 6-7]

15. Kwa nini Mashahidi wa Yehova hawasali Mungu ili akomeshe vita na ukosefu wa chakula, na ili kwamba azuie mateso yoyote? [jv uku. 317 fu. 4]

16. Ni katika njia gani Esteri alionyesha kujidhibiti (kujiweza)? [ad uku. 494 fu. 11]

17. Ijapokuwa alikuwa kuhani mkuu katika Israeli, Eli alijionyesha dhaifu kuelekea watoto wake. Ni katika njia gani alijionyesha dhaifu, na ni matokeo gani hilo liliweza kuwa nayo juu yao? (1 Sam. 2:​12, 29, 34) [ad uku. 441 maf. 7-8]

18. Daudi alikuwa akisema juu ya nani katika Zaburi 52:​2, 3 na kwa nini mtu huyo alikuwa mwenye kudharauliwa hivyo? [ad uku. 407 maf. 6-7]

19. Katika Hagai 2:​9, ni hekalu gani lilikuwa “nyumba ya mwisho,” ni gani ilikuwa ya “kale,” na kwa nini utukufu wa ile “nyumba ya mwisho” ulikuwa mkubwa zaidi kuliko ule wa ile ya “kale”? [Usomaji wa Biblia; ona wSW89 6/1 uku. 30.]

20. Ni kipa moyo gani Hosea 14:2 alitoa kwa Waisraeli, na jinsi gani Mashahidi wa Yehova wanatimiza unabii huo katika siku zetu? (Ebr. 13:15) [Usomaji wa Biblia; ona wSW94 9/15 uku. 10 maf. 1-2.]

Jaza nafasi zilizo wazi katika sentensi zifuatazo:

21. Mji wa _________________________ uliitwa mji wa mauaji na nabii _________________________ yapata miaka 200 kisha _________________________ kutimiza ndani utume wa kimungu. [siSW uku. 154 fu. 10, uku. 160 fu. 10]

22. Tunapaswa kumwabudu Mungu kwa _________________________ , tukisukumwa na moyo wenye kujaa imani na upendo; tunapaswa pia kumwabudu katika _________________________ kwa kujifunza Neno lake. [klSW uku. 45 fu. 4]

23. Nabii _________________________ alimwomba mfalme _________________________ kutayarisha mkutano pamoja na manabii 450 wa _________________________ ; ilionekana wazi kwamba Yehova ndiye Mungu wa kweli na kwamba anatoa jibu kwa _________________________ . (Yak. 5:​16, 17) [ad uku. 443 maf. 1-2]

24. Kielelezo cha Kikristo cha _________________________ , wa ukoo wa kiyahudi, na cha mwana wake _________________________ kinaonyesha kwamba inawezekana kwa wale wanaoishi katika nyumba _________________________ kufundisha kwa matokeo watoto wao kumwogopa Yehova. [ad uku. 502 fu. 2]

25. Shuhuda za aina tatu zinaonyesha kwamba Yesu alikuwa Masiya: (1) _________________________ , (2) _________________________ na (3) _________________________ . [klSW kur. 34-8 maf. 6-10]

Onyesha majibu ya kweli katika habari zifuatazo:

26. Kuelewa Amosi (8:11; 9:​2, 3; 9:​11, 12) kulisaidia Baraza linaloongoza la karne ya kwanza kutambua kwamba kukusanywa kwa wasio wayahudi katika kutaniko la Kikristo kulikuwa kwenye kulingana na mapenzi ya Mungu. (Matendo 15:​13-19) [siSW uku. 150 fu. 16]

27. Wakati (Amosi; Yoeli; Habakuki) aliitwa na Yehova, hakuwa wala nabii, wala mwana wa nabii, lakini mchungaji kondoo na mkata (mitende; tini; mizabibu) za mikuyu. (Amosi 7:14) [siSW uku. 148 fu. 1]

28. Ufufuo wa kwanza uliofanywa na mtume mmoja na unaoripotiwa katika Maandiko ulifanyika wakati (Yohana; Petro; Paulo) alipokwenda Yope ili kumwamsha (Dorkasi; Lidia; Etishi) kutoka kwa wafu. [ad uku. 411 maf. 3-4]

29. Kati ya “wafariji” watatu, (Bildadi; Elifazi; Sofari) alikuwa akisema kwanza na anaonekana kuwa ndiye aliyekuwa mwenye uvutano zaidi, jambo linalofanya kufikiri kwamba alikuwa pia labda (tajiri; mwenye hekima; mwenye umri mkubwa) zaidi. [ad uku. 445 fu. 2]

30. Ndugu pacha wa (Yosefu; Ismaeli; Yakobo) aliitwa Esau kwani alikuwa (mzaliwa wa kwanza; mwiindaji; mwenye manyoa kwa mshangao), na baadaye akachukua jina la (Nimrodi; Edomu; Baali) kwa sababu ya mlo wa chakula chekundu kupitia hicho aliuzisha haki yake ya mzaliwa wa kwanza. [ad uku. 477 fu. 4]

Patanisha habari zifuatazo na Maandiko yanayolingana nayo:

2 Fal. 2:​23, 24; Sef. 2:3; Flp. 2:​25-30; Yak. 1:​26, 27; 1 Yn. 2:​15-17.

31. Ili kwamba ibada yetu ikubaliwa na Mungu, haipaswi kuchafuliwa na matendo maovu na inapasa kutia ndani yote yaliyo ya lazima machoni pa Mungu. [klSW uku. 51 fu. 20]

32. Yehova anaomba watoto wanaojionyesha kuwa wakosa-adabu kuelekea watumishi wake waaminifu kutoa hesabu. [ad uku. 446 fu. 3]

33. Wakati na tukio lisilotazamiwa hufikia hata watumishi waaminifu wa Yehova. [ad uku. 461 fu. 8]

34. Wakristo wa kweli wanapaswa kujilinda na aina yoyote ya matendo yanayoonyesha roho ya ulimwengu mwovu unaotuzunguka. [klSW uku. 50 fu. 17]

35. Hatuwezi kuchukua vivi hivi rehema ya Mungu. [siSW uku. 165 fu. 11]

S-97-SW  Na. 290a 12/96

    Vichapo vya Swahili (Congo) (1996-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili (Congo)
    • Tumia Wengine
    • Préférences
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Kanuni za Matumizi
    • Kanuni za Kutunza Siri
    • Paramètres Kuhusu Kutunza Siri
    • JW.ORG
    • Ingia
    Tumia Wengine