Watchtower—MAKTABA KU ENTERNETE
Watchtower
MAKTABA KU ENTERNETE
Kiswahili (Congo)
  • BIBLIA
  • VICHAPO
  • MIKUTANO
  • km 12/97 uku. 3-4
  • Kujikumbusha Kwa Kuandika Kwa Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Hakuna video juu ya habari yenye umechagua.

Pole, kulikuwa kosa fulani wakati video ilikuwa inajaribu kusoma.

  • Kujikumbusha Kwa Kuandika Kwa Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1997
Huduma Yetu ya Ufalme—1997
km 12/97 uku. 3-4

Kujikumbusha Kwa Kuandika Kwa Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Kujikumbusha, vitabu vikiwa vyenye kufungwa, kwa mambo yaliyozungumzwa kwenye Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma toka Septemba 1 mpaka lile la Desemba 22, 1997. Jibu kwa kutumia karatasi tofauti kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.

[Agizo: Wakati wa kujikumbusha, tumia tu Biblia. Mitajo inayatolewa kisha kila ulizo inatolewa ili kukurahisisha utafiti wako mwenyewe. Namba za kurasa na mafungu hazionyeshwi kila mara kuhusu mitajo ya Mnara wa Mlinzi.]

Jibu Kweli au Si kweli kisha sentensi kifuatazo:

1. Ingawa habari inasema kwamba mfalme asiyekuwa mwaminifu Yehoramu alitawala ufalme wa kaskazini wa Israeli, hatujui ni nani waliokuwa wazazi wake wala namna alivyokufa. [ad 842 fu. 9, 843 fu. 2]

2. Katika Luka 22:​30, usemi “makabila kumi na mawili ya Israeli” una maana moja na ule ulio katika Mathayo 19:28 ambapo hautumiwi kuwahusu makuhani-wenzi wa Yesu waliozaliwa kwa roho, bali wanadamu wengine wote. [Usomaji wa Biblia; ona w87-SW 3/1 uku. 27 fu. 10; uku. 28 fu. 12.]

3. Wanafunzi walionyesha mshangao wao walipomuona Yesu akizungumza na mwanamke msamaria kwa sababu alikuwa na maisha yasiyo ya adili. (Yohana 4:27) [Usomaji wa Biblia; ona w95-SW 7/15 uku. 15 maf. 1-2.]

4. Katika Yohana 6:​64, usemi “kutoka mwanzo” unaonyesha kwamba, wakati Yuda alipochaguliwa kuwa mtume, Yesu alijua kwamba angemsaliti. [Usomaji wa Biblia; ona ad 868 maf. 8, 9, 869 fu. 1.]

5. Masharti (sheria) ya Sosaiti katika 1884 yalionyesha kwamba kusudi layo lilisimamia tu kwenye kazi ya uchapaji. [jv uku. 576 fu. 1]

6. Kutoka 21:​22, 23 inatuwezesha kuelewa kwamba Mungu anaona mtoto ambaye bado kuzaliwa kuwa uhai wenye thamani. [kl-SW uku. 128 fu. 21]

7. “Sikukuu ya Wayahudi” inayozungumziwa katika Yohana 5:1 ni Pasaka ya mwaka wa 31 wakati wetu wa kawaida. [si-SW uku. 194 fu. 8]

8. Ni jambo lenye matokeo pia kutangaza ujumbe wa Ufalme kwa njia ya redio na televisheni kama vile kwa njia nyingine. [jv uku. 572 fu. 2]

9. Kwa kuwa Yehoyakimu alizaa wana saba, amri ya kibiblia “andikeni habari za mutu huyu kwamba hana watoto” inapaswa kuwa ni kosa. (Yer. 22:30) [ad 766 fu. 2]

10. Wakristo wa kweli wanapaswa kuandikisha ndoa yao kwa wakuu wa serikali, iwe wanaonwa kuwa wenye haki au wasio haki. [kl-SW uku. 122 fu. 11]

Jibu maulizo yafuatayo:

11. Kulingana na kielelezo cha Wakristo wa Efeso wa karne ya kwanza, ni nini mojawapo ya hatua za kuchukua ili kupinga roho waovu? (Mdo 19:19) [kl-SW uku. 114 fu. 14]

12. Ni dhambi gani malaika fulani waliotenda katika siku za Noa? [kl-SW uku. 109 fu. 4]

13. Kwa nini Yesu alikataa kujiunga katika mzozo wa urithi? (Luka 12:​13, 14) [Usomaji wa Biblia; ona w97-SW 4/1 uku. 28.]

14. Nini ambalo wanafunzi hawakuwa wakifahamu walipomuuliza Yesu ikiwa angerudisha Ufalme kwa Israeli, kulingana na yale yanayoripotiwa na Matendo 1:6? [Usomaji wa Biblia; ona w90-SW 6/1 uku. 11 fu. 4.]

15. Kwa nini Adolf Hitler hakufaulu kutekeleza shambulio lake la kuwaangamiza watu wa Yehova? [jv uku. 553 maf. 2-4]

16. Jinsi gani Yairo alionyesha imani yake katika uwezo wa Yesu wa kuponya? (Marko 5:​22-24) [ad 747 fu. 2]

17. Kwa nini Tafsiri ya Ulimwengu Mpya inatafsiri Yohana 1:1 kwa “neno alikuwa mungu” badala ya “Neno alikuwa Mungu” kama zinavyofanya tafsiri nyingine? [Usomaji wa Biblia; ona rs-SW uku. 431 fu. 3.]

18. Kulingana na kitabu cha Ufunuo, mwisho wa wale “wanaozoea kupashana habari na roho” utakuwa nini wasipotubu na kubadili mwenendo wao? [kl-SW uku. 111 fu. 8]

19. Kwa kuwa Yesu alikuwa mwanadamu mkamilifu na kwamba alijitambua kuwa mwalimu, kwa nini alikataa kuitwa “Mwalimu mwema?” (Lk. 18:​18, 19) [Usomaji wa Biblia; ona w95-SW 3/1 uku. 15 fu. 7.]

20. Ni katika maana gani amri iliyotolewa katika Yohana 13:34 ilikuwa mpya? [Usomaji wa Biblia; ona w90-SW 2/1 uku. 21 maf. 5-6.]

Jaza nafasi zilizo wazi katika sentensi zifuatazo:

21. Kielelezo cha _________________________ , mgititi, aliyeonyesha uaminifu wake kwa _________________________ , kingepaswa kutusukuma kuonyesha sifa iyohiyo kuwaelekea wale wanaoongoza tengenezo la Yehova leo. (2 Sam. 15:21) [ad 735 fu. 6]

22. “Mina kumi” humaanisha _________________________ ambayo wanafunzi wapakwa-mafuta kwa roho wanaweza kutumia ili kufanya _________________________ zaidi wa Ufalme wa kimbingu. (Lk. 19:13) [Usomaji wa Biblia; ona w89-SW 10/1 uku. 8.]

23. Mbele ya Pilato, gavana mroma wa Yudea, Wayahudi walitunga mashtaka matatu dhidi ya Yesu, wakimshtaki kupindua _________________________ , kukataza watu wasilipe _________________________ na kusema kwamba yeye ni _________________________ . (Lk. 23:2) [Usomaji wa Biblia; ona w90-SW 12/1 uku. 9 fu. 1.]

24. Wakristo wa kweli hawasherehekei Krismasi wala sikukuu nyingine yoyote inayotokana na imani za uongo za kidini. Hawaadhimishi pia sikukuu zenye _________________________ wanadamu wasiokamilika au mataifa, kwa kuwa wanamtolea Yehova _________________________ . [kl-SW uku. 126 fu. 16]

25. Kitabu cha Matendo ya Mitume kiliandikwa na _________________________  alipokuwa _________________________ . [si-SW uku. 199 fu. 3]

Onyesha majibu ya kweli katika habari zifuatazo:

26. Katika 1992, zaidi ya wanafunzi (2,500; 4,500; 6,500) wenyeji wa nchi (40; 80; 110) walipewa mazoezi Gileadi na kutumwa katika zaidi ya nchi na visiwa (100; 150; 200). [jv uku. 524 fu. 3]

27. Katika (1887; 1879; 1881) Charles Russel alitangaza broshua The Object and Manner of Our Lord’s Return (Kusudi na namna ya kurudi kwa bwana wetu) na katika (1877; 1879; 1881) akaanza utangazaji wa Phare de la Tour de Sion et Messager de la Présence de Christ. [jv uku. 557 fu. 1]

28. Ikiwa tunaishi maisha yanayopatana na mapenzi ya Mungu, tupo hakika (kutendewa sikuzote vizuri na wengine; kuishi leo katika uwingi wa vitu vya kimwili; kujihisi wenye kukubaliwa na Mungu kwa sababu tunafanya yaliyo haki). [kl-SW uku. 118 fu. 2]

29. Kwa kumuuliza mtume Petro: “Je, wanipenda mimi kuliko hawa?” Yesu alimuuliza kwa kweli ikiwa alimpenda zaidi ya (alivyopenda wale wanafunzi wengine; namna wanafunzi hao walivyompenda; namna alivyopenda vitu vile, samaki kwa mfano) (Yohana 21:15). [Usomaji wa Biblia; ona w88-SW 11/1 uku. 31 fu. 9.]

30. Kwa watu walio wengi, wale wanaoshiriki katika mahubiri ya habari njema ni (watu matajiri; wanaume wenye kuheshimika; watu wa kawaida) [jv uku. 548 fu. 3]

Patanisha habari zifuatazo na maandiko yanayolingana nayo:

 2 Wafalme 10:​15, 16; Mit. 3:​9, 10; Lk. 9:​60, 62; 13:​4, 5; Rom. 9:​10-12

31. Yesu alishutumu fikira zenye kusema kwamba mambo yote ya maisha hupangwa kimbele kwa kuzungumzia tukio la msiba lenye kujulikana vizuri na wasikilizaji wake na kusema hilo kuwa ni matukio yasiyotazamiwa. [Usomaji wa Biblia; ona w96-SW 9/1 uku. 5 fu. 5.]

32. Yehova alionyesha kwamba alikuwa na uwezo wa kutambua mipangilio ya tabia ya mtu hata kabla ya kuzaliwa kwake na kutumia uwezo wake wa kuona mambo kimbele na haki yake ya kuchagua mapema nani anayetaka ili kutimiza makusudi yake. [ad 738 fu. 3]

33. Ni jambo la maana kuonyesha ujitoaji usiogawanyika ili kuingia katika Ufalme. [si-SW uku. 192 fu. 32]

34. Yehova atatubariki kwa kuwa tunatumia wakati wetu, nishati (nguvu) zetu, fedha zetu na mali nyingine ili kutegemeza ibada ya kweli. [kl-SW uku. 121 fu. 8]

35. Inafaa kutegemeza kiaminifu wale wanaopanga ibada inayotolewa kwa Yehova. [ad uku. 837 fu. 7]

    Vichapo vya Swahili (Congo) (1996-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili (Congo)
    • Tumia Wengine
    • Préférences
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Kanuni za Matumizi
    • Kanuni za Kutunza Siri
    • Paramètres Kuhusu Kutunza Siri
    • JW.ORG
    • Ingia
    Tumia Wengine