Watchtower—MAKTABA KU ENTERNETE
Watchtower
MAKTABA KU ENTERNETE
Kiswahili (Congo)
  • BIBLIA
  • VICHAPO
  • MIKUTANO
  • g 2/13 uku. 16
  • Mkia wa Mjusi Anayeitwa Agama

Hakuna video juu ya habari yenye umechagua.

Pole, kulikuwa kosa fulani wakati video ilikuwa inajaribu kusoma.

  • Mkia wa Mjusi Anayeitwa Agama
  • Amuka!—2013
  • Habari za Kufanana na Zile
  • Yaliyomo
    Amuka!—2013
  • Mujusi wa Miiba-Miiba Mwenye Ngozi Yenye Kukokota Maji
    Amuka!—2015
  • Habari Zilizo Ndani
    Amuka!—2015
Amuka!—2013
g 2/13 uku. 16
[Picha katika ukurasa wa 16]

JE, NI KAZI YA UBUNI?

Mkia wa Mjusi Anayeitwa Agama

MJUSI anayeitwa agama huruka kutoka mahali tambarare hadi ukutani bila matatizo yoyote. Lakini iwapo mahali tambarare ni laini, mjusi huyo huteleza lakini bado anafaulu kuruka na kujishikilia ukutani. Anafanyaje hivyo? Siri ya mjusi huyo ni mkia wake.

Fikiria hili: Mijusi hao wanaporuka kutoka kwenye eneo tambarare lenye mikwaruzo​—ambalo huwasaidia kujishikilia vizuri—​kwanza wao husawazisha miili yao na kuhakikisha mkia wao umelala chini. Hilo huwawezesha kuruka kwa pembe inayofaa. Hata hivyo, mijusi hao wanapokuwa kwenye sehemu laini, wao huteleza na kuruka kwa pembe isiyofaa. Lakini wakiwa hewani, wao husawazisha mwili wao inavyofaa kwa kurusha mkia wao juu. Hawafanyi hivyo ovyoovyo tu. “Lazima mijusi hao wabadili pembe ya mkia wao kwa njia inayofaa kabisa ili waendelee kuwa wima,” inasema ripoti moja iliyotolewa na Chuo Kikuu cha California, Berkeley. Kadiri sehemu anayokanyaga ilivyo na utelezi ndivyo mjusi huyo anavyolazimika kuinua mkia wake ili atue kwa njia inayofaa.

Mkia wa mjusi huyo unaweza kuwasaidia mainjinia kubuni magari ya roboti yasiyoanguka kwa urahisi ambayo yanaweza kutumiwa kuwatafuta waokokaji baada ya tetemeko la nchi au msiba mwingine. “Roboti hazina uwezo wa kujisawazisha kama wanyama,” anasema mtafiti Thomas Libby, “kwa hiyo, chochote kinachoweza kuzifanya ziwe imara zaidi ni maendeleo.”

Una maoni gani? Je, mkia wa mjusi anayeitwa agama ulijitokeza wenyewe? Au ulibuniwa?

    Vichapo vya Swahili (Congo) (1996-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili (Congo)
    • Tumia Wengine
    • Préférences
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Kanuni za Matumizi
    • Kanuni za Kutunza Siri
    • Paramètres Kuhusu Kutunza Siri
    • JW.ORG
    • Ingia
    Tumia Wengine