Vidio Iliyo na Ujumbe Wenye Kudumu
Ni ujumbe gani ulio katika vidio David : il mettait sa confiance en Dieu ? (Daudi: Alimtegemea Mungu?) Kama Daudi, tunapaswa kumtegemea Yehova. (Zab. 91:2) Kwa kutazama matukio ya maana ya maisha ya Daudi yanayozungumziwa katika vidio hiyo, kutasaidia watoto na watu wazima kujifunza kutokana na mfano alioutoa. (Zab. 31:14) Ili itufaidi zaidi, DVD hii inatia ndani “Maulizo” na “Mambo Mbalimbali Yenye Kufundisha.”
Tazama vidio, na kisha ujiulize: (1) Kwa nini Yehova alichagua mfalme bora? (1 Sam. 15:10, 11; 16:1) (2) Kwa nini hakuchagua yeyote kati ya ndugu za Daudi? (1 Sam. 16:6, 7) (3) Kwa nini Saulo alipenda Daudi apige kinubi? (1 Sam. 16:14-23) (4) Goliathi alikuwa nani? (1 Sam. 17:4-10) (5) Kwa nini Daudi alipenda kumpiganisha Goliathi? (1 Sam. 17:23, 24, 36, 37) (6) Yonathani alikuwa nani? (1 Sam. 14:1) (7) Ni kwa kiasi gani Saulo alikuja kuwa adui mkubwa zaidi wa Daudi? (1 Sam. 18:25-29) (8) Kwa nini Daudi hakumuua Saulo? (1 Sam. 26:7-11)
(9) Saulo alikufa namna gani? (1 Sam. 31:1-6)
(10) Itikio la Daudi lilikuwa nini kuhusu kifo cha Yonathani? (2 Sam. 1:11, 12)
(11) Ni ahadi gani ambayo Yehova alimtolea Daudi? (2 Sam. 7:12, 13, 16) (12) Ni kosa gani nzito ambalo Daudi alifanya? (2 Sam. 11:1-5, 14-17) (13) Daudi alionyeshaje kwamba alihuzunika sana kwa sababu ya jambo alilofanya? (Zab. 51) (14) Ni somo gani mbalimbali ambazo Daudi alimfundisha kijana Solomono? (1 Fal. 2:1-4; 1 Nya. 22:6-13; 28:9, 10) (15) Namna gani utawala wa Yesu utafaidi Daudi, Yonathani, na wewe?—Isa. 11:6-9; Yoh. 11:25, 26.
Sasa fikiri kwa uzito: Daudi alimtegemea Mungu; unawezaje kibinafsi kuiga jambo hilo?
Wazazi, mkazie katika watoto wenu umaana wenye kudumu wa kumtumaini Mungu, kama Daudi alivyofanya.—Zab. 56:11.