Waebrania
Kwa Waebrania
1 Mungu, ambaye zamani za kale katika vipindi vingi na katika njia nyingi alisema na baba zetu wa zamani kwa njia ya manabii, 2 mwishoni mwa siku hizi amesema nasi kwa njia ya Mwana, aliyemweka rasmi kuwa mrithi wa vitu vyote, na ambaye kupitia yeye aliifanya mifumo ya mambo. 3 Yeye ndiye mrudisho wa utukufu wake na mwakilisho sawasawa wa utu wake wenyewe, naye hutegemeza vitu vyote kwa neno la nguvu yake; na akiisha kufanya utakaso wa dhambi zetu aliketi kwenye mkono wa kuume wa Ukuu katika mahali palipoinuka sana. 4 Kwa hiyo amekuwa bora kuliko malaika, kwa kadiri ambayo amerithi jina bora kabisa kuliko lao.
5 Kwa kielelezo, ni yupi kati ya malaika ambaye yeye alimwambia wakati wowote: “Wewe ni mwana wangu; mimi, leo, nimekuwa baba yako”? Na tena: “Mimi mwenyewe nitakuwa baba yake, naye mwenyewe atakuwa mwana wangu”? 6 Lakini amwingizapo tena Mzaliwa wake wa kwanza katika dunia inayokaliwa, yeye asema: “Na acheni malaika wote wa Mungu wamsujudu.”
7 Pia, kuhusu malaika yeye asema: “Naye hufanya malaika zake kuwa roho, na watumishi wake wa watu wote kuwa mwali wa moto.” 8 Lakini kuhusu Mwana: “Mungu ni kiti chako cha ufalme milele na milele, na gongo la utawala la ufalme wako ndilo gongo la utawala wa unyoofu. 9 Wewe ulipenda uadilifu, nawe ulichukia uasi-sheria. Hiyo ndiyo sababu Mungu, Mungu wako, alikutia mafuta ya mchachawo zaidi ya wenzako.” 10 Na: “Wewe katika mwanzo, Ee Bwana, uliweka misingi ya dunia yenyewe, na mbingu ni kazi za mikono yako. 11 Hizo zenyewe zitaangamia, lakini wewe mwenyewe ni wa kubaki kwa kuendelea; na sawasawa na vazi la nje zote zitachakaa, 12 nawe utazikunja kama vile joho, kama vazi la nje; nazo zitabadilishwa, lakini wewe ni yuleyule, nayo miaka yako haitaisha kamwe.”
13 Lakini ni kuhusu yupi kati ya malaika amesema wakati wowote: “Keti kwenye mkono wangu wa kuume, mpaka niweke maadui wako kama kibago kwa ajili ya miguu yako”? 14 Je, wao wote si roho kwa ajili ya utumishi wa watu wote, waliotumwa kuwahudumia wale watakaorithi wokovu?