19 Siku saba unga wowote uliokandwa wenye chachu usipatikane katika nyumba zenu, kwa sababu mtu yeyote anayeonja kitu kilicho na chachu, awe mkaaji mgeni au mwenyeji wa nchi,+ nafsi hiyo itakatiliwa mbali kutoka katika kusanyiko la Israeli.+
48 Na ikiwa mkaaji mgeni anakaa pamoja nawe akiwa mgeni naye atasherehekea pasaka kwa Yehova, kila mwanamume wa kwake na atahiriwe.+ Ndipo apate kukaribia ili kuisherehekea; na awe kama mwenyeji wa nchi. Bali mwanamume yeyote ambaye hajatahiriwa asipate kuila.