22 Nanyi mtachukua tawi la hisopo+ na kulichovya katika damu iliyo ndani ya beseni na kuipaka sehemu ya juu ya mlango na juu ya ile miimo miwili ya mlango kwa kiasi fulani cha damu iliyo kwenye beseni; na yeyote kati yenu asitoke nje ya mlango wa nyumba yake mpaka asubuhi.