10 Tena akajenga minara+ nyikani, na kuchimba matangi mengi ya maji (kwa maana alikuwa na mifugo mingi sana), na pia katika Shefela+ na katika nchi tambarare ya juu. Palikuwa na wakulima na watunza-mizabibu katika milima na katika Karmeli, kwa maana alipenda kilimo.