2 Na ikawa kwamba, mara tu mfalme alipomwona Malkia Esta amesimama katika ua, akapata kibali+ machoni pake, naye mfalme akamnyooshea Esta fimbo yake ya enzi ya dhahabu+ iliyokuwa mkononi mwake. Basi Esta akakaribia na kuigusa ncha ya fimbo hiyo ya enzi.