21 Siku hizo Mordekai alipokuwa anaketi katika lango la mfalme, Bigthani na Tereshi, maofisa wawili wa makao ya mfalme, watunza-milango, waligadhibika nao wakazidi kutafuta kumdhuru+ Mfalme Ahasuero.
10 Mara moja mfalme akamwambia Hamani: “Fanya haraka, chukua mavazi na farasi, kama ulivyosema, umfanyie hivyo Mordekai yule Myahudi anayeketi katika lango la mfalme. Usiache jambo lolote likose kutimia kati ya mambo yote uliyoyasema.”+