2 Na watumishi wote wa mfalme waliokuwa katika lango la mfalme+ walikuwa wanainama na kumsujudia Hamani, kwa maana mfalme alikuwa ametoa amri hiyo kumhusu. Lakini Mordekai hakuinama wala kusujudu.+
4 Baadaye mfalme akasema: “Ni nani aliye katika ua?” Basi Hamani alikuwa amekuja katika ua wa nje+ wa nyumba ya mfalme ili kumwambia mfalme kwamba Mordekai atundikwe juu ya mti+ ambao alikuwa amemwekea tayari.