-
Mwanzo 41:18-21Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
18 Na tazama! ng’ombe saba wazuri, walionona, walikuwa wakipanda kutoka katika Mto Nile, wakaanza kula nyasi za Mto Nile.+ 19 Baada yao, ng’ombe wengine saba dhaifu, wenye sura mbaya sana, na waliokonda walipanda kutoka katika Mto Nile. Sijawahi kamwe kuona ng’ombe wenye sura mbaya hivyo katika nchi yote ya Misri. 20 Na ng’ombe hao waliokonda, wenye sura mbaya, wakaanza kuwala wale ng’ombe saba wa kwanza walionona. 21 Lakini baada ya kuwala, hakuna yeyote angejua kwamba wamewala ng’ombe hao, kwa kuwa sura yao ilikuwa mbaya kama mwanzoni. Ndipo nikaamka.
-