-
Mwanzo 41:2-4Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
2 Na tazama! ng’ombe saba wazuri, walionona, walikuwa wakipanda kutoka mtoni, nao walikuwa wakila nyasi za Mto Nile.+ 3 Baada yao, ng’ombe wengine saba wenye sura mbaya na waliokonda walipanda kutoka katika Mto Nile, wakasimama karibu na wale ng’ombe wanono kwenye ukingo wa Mto Nile. 4 Kisha wale ng’ombe wenye sura mbaya, waliokonda, wakaanza kuwala wale ng’ombe saba wazuri, walionona. Ndipo Farao akaamka.
-