-
Mwanzo 41:5-7Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
5 Kisha akarudi kulala, akaota ndoto ya pili. Kulikuwa na masuke saba ya nafaka yakitokea katika bua moja, yalikuwa yamejaa nafaka nayo yalikuwa mazuri sana.+ 6 Na baada ya hayo, masuke mengine saba ya nafaka yakakua, yalikuwa membamba na yalikuwa yamechomwa na upepo wa mashariki. 7 Kisha masuke hayo membamba ya nafaka yakaanza kuyameza yale masuke saba ya nafaka yaliyojaa nafaka na ambayo yalikuwa mazuri sana. Ndipo Farao akaamka na kugundua kwamba ilikuwa ndoto.
-