-
Mwanzo 37:31-34Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
31 Basi wakalichukua joho la Yosefu, wakamchinja mbuzi dume na kulichovya joho hilo katika damu ya mbuzi huyo. 32 Kisha wakamtumia baba yao joho hilo na kumwambia: “Hiki ndicho tulichopata. Tafadhali chunguza uone ikiwa joho hili ni la mwanao au la.”+ 33 Basi akalichunguza na kusema kwa mshtuko: “Ni joho la mwanangu! Inaonekana ameliwa na mnyama mkali wa mwituni! Kwa hakika Yosefu ameraruliwa vipandevipande!” 34 Ndipo Yakobo akayararua mavazi yake na kuvaa nguo za magunia kiunoni na kumwombolezea mwanawe kwa siku nyingi.
-