11 Yuda akamwambia Tamari binti mkwe wake: “Ishi ukiwa mjane katika nyumba ya baba yako mpaka Shela mwanangu atakapokua,” kwa maana Yuda alisema moyoni mwake: ‘Huenda yeye pia akafa kama ndugu zake.’+ Basi Tamari akaenda kuishi katika nyumba ya baba yake.
5 “Ikiwa ndugu wanaishi pamoja na mmoja wao afe bila mwana, mke wa yule aliyekufa hapaswi kuolewa na mwanamume mwingine nje ya ukoo huo. Ndugu ya mume wake anapaswa kwenda kwake, amchukue awe mke wake, na kufunga naye ndoa ya ndugu mkwe.+