-
Kutoka 25:23-28Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
23 “Pia utatengeneza meza+ ya mbao za mshita yenye urefu wa mikono miwili na upana wa mkono mmoja na kimo cha mkono mmoja na nusu.+ 24 Utaifunika kwa dhahabu safi na kutengeneza ukingo wa dhahabu kuizunguka. 25 Utatengeneza utepe wenye upana wa kiganja kimoja* kuizunguka na ukingo wa dhahabu kuzunguka utepe huo. 26 Utaitengenezea pete nne za dhahabu na kuzitia kwenye pembe nne za miguu yake minne, sehemu ambazo miguu hiyo minne inaungana na meza. 27 Pete hizo zitakuwa karibu na utepe ili zitiwe fito za kubebea meza hiyo. 28 Utatengeneza fito za mshita na kuzifunika kwa dhahabu, nanyi mtazitumia kubebea meza hiyo.
-