Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutoka 28:15-21
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 15 “Utamwagiza fundi wa kutarizi atengeneze kifuko cha kifuani cha maamuzi.+ Atakitengeneza kama efodi, kwa kutumia dhahabu, nyuzi za bluu, sufu ya zambarau, kitambaa cha rangi nyekundu, na kitani bora kilichosokotwa.+ 16 Kifuko hicho kinapaswa kuwa cha mraba kinapokunjwa mara mbili, urefu wake uwe shubiri moja* na upana wake shubiri moja. 17 Unapaswa kuweka kwenye kifuko hicho mawe yaliyopangwa katika safu nne. Safu ya kwanza itakuwa na zabarijadi, topazi, na zumaridi. 18 Safu ya pili itakuwa na feruzi, yakuti, na yaspi. 19 Safu ya tatu itakuwa na jiwe la leshemi,* akiki, na amethisti. 20 Safu ya nne itakuwa na krisolito, shohamu, na yashefi. Mawe hayo yatawekwa kwenye vifuko vya dhahabu. 21 Mawe hayo yatalingana na majina 12 ya wana wa Israeli. Kila jina linapaswa kuchongwa kama muhuri unavyochongwa, na kila jina litawakilisha mojawapo ya makabila 12 ya wana wa Israeli.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki