Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutoka 39:8-14
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 8 Kisha akatengeneza kifuko cha kifuani+ na kukitarizi. Akakitengeneza kama efodi kwa kutumia dhahabu, nyuzi za bluu, sufu ya zambarau, kitambaa cha rangi nyekundu, na kitani bora kilichosokotwa.+ 9 Kifuko hicho kilikuwa cha mraba kilipokunjwa mara mbili. Walikitengeneza kifuko hicho cha kifuani kikiwa na urefu wa shubiri moja* na upana wa shubiri moja kinapokunjwa mara mbili. 10 Wakaweka kwenye kifuko hicho mawe yaliyopangwa katika safu nne. Safu ya kwanza ilikuwa na zabarijadi, topazi, na zumaridi. 11 Safu ya pili ilikuwa na feruzi, yakuti, na yaspi. 12 Safu ya tatu ilikuwa na jiwe la leshemi,* akiki, na amethisti. 13 Safu ya nne ilikuwa na krisolito, shohamu, na yashefi. Mawe hayo yaliwekwa kwenye vifuko vya dhahabu. 14 Yalilingana na majina 12 ya wana wa Israeli, na majina hayo yalichongwa kama muhuri, na kila jina liliwakilisha mojawapo ya makabila 12 ya wana wa Israeli.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki