-
Kutoka 28:22-25Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
22 “Utakitengenezea kifuko cha kifuani minyororo iliyosokotwa, kama kamba za dhahabu safi.+ 23 Pia utakitengenezea pete mbili za dhahabu na kuzitia kwenye pembe mbili za juu za kifuko hicho. 24 Utatia zile kamba mbili za dhahabu katika pete mbili zilizo kwenye pembe za kifuko cha kifuani. 25 Kisha utatia ncha mbili za zile kamba mbili katika vile vifuko viwili vya mabegani, nawe unapaswa kuzifunga ncha hizo kwenye vipande viwili vya efodi, sehemu ya mbele.
-