-
Kutoka 39:15-18Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
15 Kisha wakakitengenezea kifuko cha kifuani minyororo iliyosokotwa, kama kamba za dhahabu safi.+ 16 Halafu wakatengeneza vifuko viwili vya dhahabu na pete mbili za dhahabu na kuzitia kwenye pembe mbili za juu za kifuko hicho. 17 Baada ya hayo wakatia zile kamba mbili za dhahabu katika pete mbili zilizo kwenye pembe hizo. 18 Kisha wakatia ncha mbili za hizo kamba mbili katika vile vifuko viwili vya mabegani na kuzifunga ncha hizo kwenye vipande viwili vya efodi, sehemu ya mbele.
-