-
Kutoka 36:14-18Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
14 Kisha akatengeneza vitambaa vya manyoya ya mbuzi vya kufunika hema hilo. Akatengeneza vitambaa 11 vya hema.+ 15 Kila kitambaa kilikuwa na urefu wa mikono 30 na upana wa mikono 4. Vitambaa vyote 11 vilikuwa na ukubwa uleule. 16 Kisha akaunganisha vitambaa vitano pamoja na vile vitambaa vingine sita pamoja. 17 Halafu akatengeneza vitanzi 50 kwenye upindo wa kitambaa cha kwanza, kwenye kipande cha mwisho kabisa, na vitanzi 50 kwenye upindo wa kitambaa cha pili, mahali vinapounganishwa. 18 Naye akatengeneza vibanio 50 vya shaba vya kuunganisha hema pamoja ili liwe na kitambaa kimoja kizima.
-