-
Kutoka 38:1-7Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
38 Akatumia mbao za mshita kutengeneza madhabahu ya dhabihu za kuteketezwa. Ilikuwa ya mraba, yenye urefu wa mikono mitano,* upana wa mikono mitano, na kimo cha mikono mitatu.+ 2 Kisha akatengeneza pembe kwenye ncha zake nne. Pembe hizo zilikuwa sehemu ya hiyo madhabahu. Naye akaifunika kwa shaba.+ 3 Baada ya hayo akatengeneza vyombo vyote vya madhabahu: ndoo za kuondolea majivu, sepetu, mabakuli, nyuma,* na vyetezo. Alitengeneza vyombo hivyo vyote kwa shaba. 4 Pia, alitengeneza wavu wa shaba kwa ajili ya madhabahu, chini ya ukingo wake, katikati ya madhabahu. 5 Alitengeneza pete nne kwenye pembe nne za wavu huo karibu na wavu huo wa shaba, ili zishikilie fito. 6 Baada ya hayo akatengeneza fito kwa mbao za mshita na kuzifunika kwa shaba. 7 Kisha akazitia fito hizo kwenye zile pete zilizo kwenye pande za madhabahu ili zitumiwe kubebea madhabahu. Alitengeneza madhabahu hiyo kama sanduku la mbao lenye uwazi.
-