Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutoka 27:1-8
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 27 “Utatengeneza madhabahu kwa mbao za mshita;+ itakuwa na urefu wa mikono mitano* na upana wa mikono mitano. Madhabahu hiyo itakuwa ya mraba na kimo chake kitakuwa mikono mitatu.+ 2 Utatengeneza pembe+ kwenye ncha zake nne; pembe hizo zitakuwa sehemu ya madhabahu, nawe utaifunika madhabahu hiyo kwa shaba.+ 3 Utatengeneza ndoo za kuondolea majivu,* pia sepetu, mabakuli, nyuma,* na vyetezo; utatengeneza vyombo vyote vya madhabahu kwa shaba.+ 4 Nawe utatengeneza wavu wa shaba kwa ajili ya madhabahu, pia utatengeneza pete nne za shaba kwenye pembe nne za wavu huo. 5 Nawe utauweka wavu huo chini ya ukingo wa madhabahu, nao utashuka ndani ya madhabahu kufikia katikati. 6 Utatengeneza fito za mshita kwa ajili ya madhabahu na kuzifunika kwa shaba. 7 Fito hizo zitaingizwa kwenye zile pete ili ziwe katika pande mbili za madhabahu wakati inapobebwa.+ 8 Utaitengeneza madhabahu hiyo kama sanduku la mbao lenye uwazi. Inapaswa kutengenezwa kama tu Alivyokuonyesha mlimani.+

  • Kutoka 40:10
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 10 Utatia mafuta madhabahu ya dhabihu za kuteketezwa pamoja na vyombo vyake vyote na kuitakasa, ili iwe madhabahu takatifu zaidi.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki