-
Kutoka 39:2-5Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
2 Alitengeneza* efodi+ kwa dhahabu, nyuzi za bluu, sufu ya zambarau, kitambaa cha rangi nyekundu, na kitani bora kilichosokotwa. 3 Walitengeneza mabamba membamba ya dhahabu kwa kutumia nyundo, naye akayakata yakawa nyuzi nyembamba ili zifumwe pamoja na zile nyuzi za bluu, sufu ya zambarau, kitambaa cha rangi nyekundu, na kitani bora, akatarizi efodi. 4 Wakatengeneza vipande vya mabegani vilivyoungana, navyo vikaunganishwa kwenye miisho miwili ya efodi. 5 Mshipi uliofumwa unaoshikilia kwa nguvu efodi ulitengenezwa kwa vitu hivyohivyo,+ yaani, dhahabu, nyuzi za bluu, sufu ya zambarau, kitambaa cha rangi nyekundu, na kitani bora kilichosokotwa, kama Yehova alivyomwamuru Musa.
-